2 Oktoba 2025 - 13:56
“Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu: FIFA na UEFA waifungie Israel”

Shirika la Amnesty International limewaomba Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), kwa kuzingatia uhalifu wa miaka miwili wa Israel katika Ukanda wa Gaza, wachukue hatua haraka dhidi ya Israel.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (Amnesty International) limetoa wito kwa FIFA na UEFA wazifungie timu za soka za Israel kushiriki mashindano ya kimataifa.

Katika barua yake, Shirika la Amnesty limeandika kuwa kwa kuzingatia uhalifu wa miaka miwili wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ni lazima UEFA na FIFA wachukue hatua haraka.

Barua hiyo ilielekezwa kwa Alexander Ceferin, Rais wa UEFA, na Gianni Infantino, Rais wa FIFA, na imesainiwa na Agnes Callamard, Rais wa Amnesty International. Katika barua hiyo, imeelezwa kuwa kulingana na kifungu cha 64.2 cha Kanuni za FIFA, taasisi hiyo inapaswa kutoa mwitikio dhidi ya uhalifu wa Israel.

Hata hivyo, vyombo vya habari vimeripoti kuwa leo Baraza la FIFA linatarajiwa kukutana, lakini kutokana na ushawishi wa lobby za Kizayuni na Rais wa Marekani, Donald Trump, inaonekana kuwa mada ya kuchunguza uhalifu wa utawala wa Israel imeondolewa kwenye ajenda, ingawa ajenda rasmi bado haijachapishwa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha