Mapambo hayo yamewekwa katika uga wa haram, njia za waumini, na maeneo ya ibada kama ishara ya: 1_Furaha ya Kiislamu, 2_Upendo kwa Ahlul-Bayt (a.s), 3_Na heshima kubwa kwa binti wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Baghdad - Iraq | Haram takatifu ya Maimamu wawili watukufu, Imam Muhammad Al-Jawad (a.s) na Imam Ali Al-Hadi (a.s), iliyopo katika mji wa Kadhimiyah, Baghdad – Iraq, imepambwa kwa maua maridadi na mapambo ya furaha kwa ajili ya kuukaribisha msimu mtukufu wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mwanamke bora zaidi kuliko Wanawake wote wa Ulimwengu mzima, Sayyidat Fatima Zahra (a.s), Binti Kipenzi wa Mtume Muhammad (saww).
Mapambo hayo yamewekwa katika uga wa haram, njia za waumini, na maeneo ya ibada kama ishara ya:
1_Furaha ya Kiislamu
2_Upendo kwa Ahlul-Bayt (a.s)
3_Na heshima kubwa kwa binti wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Waumini wengi wameendelea kufika kwa wingi kutoa:
1_Ziyara
2_Dua
3_Na kushiriki katika shamrashamra za kiroho kuelekea kumbukumbu ya tukio hilo tukufu.
Sherehe hizi huambatana pia na:
1_Majlisi za mawaidha
2_Qasida na tenzi za mapenzi kwa Bibi Zahra (a.s)
3_Na matendo ya hisani kwa wahitaji.

Your Comment