Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Wizara ya Afya ya Ghaza imetoa taarifa na kutangaza kuwa katika muda wa mchana na usiku uliopita, utawala ghasibu wa Kizayuni ulishambulia kwa mabomu maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza.
Katika taarifa hiyo imeelezwa kuwa katika muda wa saa 24 zilizopita Wapalestina 86 waliuawa Shahidi katika Mashambulizi ya Utawala gahasibu wa Kizayuni na watu 287 kujeruhiwa.
Wizara imesisitiza kuwa bado kuna idadi ya wahasiriwa chini ya vifusi na mitaani, na timu za uokoaji na zima moto haziwezi kuwafikia.
Kwa mujibu wa ripoti hii, idadi ya Mashahidi huko Gaza tangu Machi 18, 2025 imefikia watu 1,249 na idadi ya waliojeruhiwa imefikia watu 3,222.
Wizara ya Afya ya Ghaza ilizidi kutangaza kuwa kutokana na kuendelea kwa Mashambulizi ya utawala ghasibu wa Kizayuni tangu tarehe 7 Oktoba 2023, jumla ya Mashahidi wa vita hivyo imeongezeka na kufikia 50,609 na idadi ya waliojeruhiwa imeongezeka na kufikia 115,063.
Mashambulizi haya yamezidishwa huku Jumuiya ya Kimataifa na juu yake zikiwa ni Taasisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa zikionya kuhusu hali mbaya ya Kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
Your Comment