Kufuatia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) dhidi ya msafara wa kimataifa wa Sumuud (Jina la Msafara), ambao unalenga kupeleka misaada ya kibinadamu kwa Gaza na ulikuwa ukisafiri katika maji ya kimataifa, Italia na Uhispania zimetuma meli zao za kivita ili kuhakikisha usalama wa msafara huo. Hatua hii imechukuliwa baada ya kulaaniwa kwa kiwango kikubwa kwa mashambulizi hayo dhidi ya meli zisizo za kijeshi, ambayo yamechukuliwa kuwa ni uvunjaji wa sheria za kimataifa.
Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuuawa Shahidi na kujeruhiwa Wapalestina 373 katika muda wa saa 24 zilizopita na kuongezeka kwa idadi ya Mashahidi wa mauaji ya kimbari na kufikia zaidi ya watu 50,600.