20 Mei 2025 - 00:44
Kiongozi wa Kishia wa Pakistan: Safari ya Rais wa Marekani katika Nchi za Kiarabu ni Dhihaka kwa Mafundisho ya Kiislamu na Heshima ya Kiislamu

Katibu Mkuu wa Wafaq ul-Madaris al-Shia wa Pakistan, Hujjatul Islam Muhammad Afzal Haidari, alielezea masikitiko yake juu ya mapokezi yaliyotolewa na nchi za Kiarabu kwa Rais wa Marekani. Alisema kuwa njia iliyotumika kumkaribisha mtu mwenye kuuhami utawala wa Kizayuni, ni ya aibu na ni dhihaka kwa mafundisho ya Kiislamu na Heshima ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (as) -ABNA-Hujjatul Islam Muhammad Afzal Haidari alisema: "Mapokezi yaliyotolewa kwa Rais wa Marekani, ambaye ni mtu mwenye kuhami na msaidizi mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni, ni jambo la fedheha kubwa. Hili linaonyesha kuwa mshikamano wa Kiislamu, udugu, na thamani za Kiislamu miongoni mwa Waislamu zimepungua kwa kiasi kikubwa."

Aliongeza kusema: "Mapokezi ya Trump yalikuwa ni fedheha kwa damu ya watoto, mama, dada na wananchi wasio na hatia wa Palestina waliouawa na utawala haramu wa Kizayuni. Mapokezi hayo yalionesha kuwa kwa baadhi ya tawala, kinachowahimu ni mali na madaraka tu."

Katika hotuba yake katika Hawza ya Jamea al-Muntazir, Haidari alizitaka nchi za Kiislamu kutoshirikiana na utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa: "Nchi nyingine za Kiislamu zinapaswa kuonyesha heshima yao kwa Uislamu na kuungana pamoja ili kuunda mpango wa pamoja wa kuisaidia Palestina. Vinginevyo, yatawakuta yale yale yaliyowakuta watu wa Libya, Afghanistan, Iraq, Yemen na Syria – wataangamizwa mmoja baada ya mwingine."

Mwanazuoni huyo mashuhuri pia aligusia sera za unafiki za Marekani na kusema: "Marekani ilitangaza zawadi kwa kichwa cha kiongozi wa serikali ya muda ya Syria, lakini baada ya kiongozi huyo kushirikiana katika kuangamiza serikali iliyokuwa ikiisaidia Palestina na kuunda serikali inayopendelea Israel, si tu kuwa zawadi hiyo iliondolewa, bali pia vikwazo dhidi ya Syria viliondolewa. Hii inaonyesha kuwa hata gaidi, akifanya kazi kwa maslahi ya Marekani, hukubaliwa; lakini raia wa amani anayepinga Israel na kuunga mkono Palestina huchukuliwa kuwa adui."

Mwisho, alisema: "Ni aibu kubwa kwamba Marekani na washirika wake wanazungumza kuhusu haki za wanyama, lakini hawathamini damu ya Wapalestina."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha