Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema nchi yake inahitaji kuwa na mazungumzo magumu na wale wote wanaofadhili ugaidi pamoja na itikadi kali ikiwemo serikali za kigeni sambamba na washirika wake ikihitajika.
Misri imetoa masaa 48 kwa balozi wa Qatar kuondoka nchini humo na kuwaita nyumbani wawakilishi wake waandamizi waliopo Doha. Hii ni kulingana na duru za wizara ya masuala ya kigeni ya Misri
Mwito huu unafuatia hatua ya mataifa kadhaa ya Kiarabu, kutangaza kukata ushirikiano wa kidiplomasia na Qatar.