Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Khawaja Asif, Waziri wa Ulinzi wa Pakistan, katika mahojiano ya televisheni alisisitiza kuwa Osama bin Laden alikuwa "zao la Marekani", na aliletwa binafsi na mkuu wa wakati huo wa CIA kutoka Sudan. Akizungumzia mabadiliko ya kisiasa ya hivi karibuni katika eneo hilo, Asif alisema: “Shambulio la Israel dhidi ya Qatar lilifanyika kwa ridhaa ya Marekani, na Waislamu wanapaswa kulitambua hili waziwazi na kutofautisha kati ya wanaojifanya marafiki na maadui wa kweli.”
Asif aliongeza kuwa:
“Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuunda umoja wa kijeshi kama NATO. Ingawa sikukatishwa tamaa na mkutano wa nchi za Kiislamu, ukweli ni kwamba uongozi wa Hamas ulikuwepo Qatar kwa matakwa ya Marekani, na shambulio la hivi karibuni lilifanyika kwa idhini ya Washington. Hili ni tukio kubwa na athari zake zitachukua muda kuonekana, lakini bila shaka litakuwa na madhara ya muda mrefu.”
Waziri huyo pia alibainisha kuwa:
“Tusidanganyike – matukio haya yote yanafanyika kwa idhini ya Marekani. Hata huko Syria, serikali iliyopo ilikuja kwa ridhaa ya Marekani, lakini bado Israel inaishambulia.”
Katika sehemu ya mwisho ya mahojiano hayo, Asif alisema:
“Kwa sasa, kuna wimbi la hasira ya umma dhidi ya Israel nchini Marekani na mataifa ya Magharibi. Mabadiliko haya ya mitazamo ya raia huenda yakawa tishio kubwa zaidi kwa Tel Aviv kuliko kinachoendelea vitani uwanjani.”
Your Comment