Ulimwengu
-
Sayyid al-Houthi: Yemen ni nchi ya kwanza katika ulimwengu wa Kiarabu kutengeneza silaha zake za kijeshi
""Dunia sasa imeutambua utawala wa Kizayuni kuwa ni utawala wa kinyama lakini ulioshindwa"
"Hatuwezi kukaa kimya wakati wowote, na kwa namna yoyote hatutafanya biashara au kutoa punguzo juu ya msimamo wetu wa kimsingi wa kiimani, wa jihadi na wa Koran. Taifa letu linatenda kwa mujibu wa maagizo ya Mungu."
-
Kumbukumbu Maalum:
Ukimya wa Kifo wa Nchi za Kiislamu; Asia ya Magharibi, “Palestina Mpya”
Kukubaliana kwa baadhi ya nchi za Kiislamu na mpango wa kinachoitwa mpango wa amani wa Trump kuhusu Palestina, ni alama ya aibu juu ya ulimwengu wa Kiislamu na baadhi ya viongozi wao wasio na imani ya kweli, na aibu hii haitafutika hadi Siku ya Kiyama.
-
Watu Wema Hawafi: Daima Huishi katika Ulimwengu Mpana na ulio bora zaidi wa Kiroho
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu watu hawa Wema kwa rehema Zake zisizo na kikomo, na awajaalie makazi yao pamoja na Mtume Muhammad (rehema na amani zimshukie yeye) na Ahlul-Bayt wake watukufu na watoharifu (as).
-
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan: Osama bin Laden alikuwa zao la Amerika / Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuunda Muungano sawa na NATO
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan alisema: "Shambulio la Israel dhidi ya Qatar lilifanyika kwa ridhaa ya Amerika, na Waislamu wanapaswa kuelewa ukweli huu na kutofautisha kati ya "Marafiki bandia na maadui wa kweli."
-
Bi Mujtahida Saffati: Vyuo vya kidini vya wanawake vinapaswa kuchukua uongozi wa kielimu wa wanawake katika ulimwengu wa Kiislamu
Profesa mashuhuri wa vyuo vya kidini vya wanawake, katika hafla ya uzinduzi wa mwaka mpya wa masomo, alivitaja “ikhlasi na uchamungu (taqwa)”, “kuungana na uongozi wa Kiislamu (wilaya)”, na “kuzingatia haki za wengine” kuwa ni nguzo tatu muhimu za mafanikio kwa wanafunzi wa fani za dini. Akaeleza kwa msisitizo kuwa: Taasisi za kielimu za wanawake zinapaswa kuchukua uongozi wa kielimu kwa wanawake wa ulimwengu wa Kiislamu, na kutumia uwezo huo kwa ajili ya kusambaza maarifa ya Kiislamu katika ulimwengu mzima wa Kiislamu.
-
Arubaini Iwe Sauti ya Umoja wa Kiislamu na Upinzani (Muqawamah) Dhidi ya Ubeberu na Uistikbari wa Kimataifa - Rais wa Waqfu Iran
“Arubaini ya mwaka huu inapaswa kuleta tumaini kwa Waislamu na kuwavunja nguvu maadui. Umoja ndiyo njia ya wokovu kwa Ulimwengu wa Kiislamu na Bendera ya Mapambano dhidi ya mfumo wa kishetani lazima ibaki juu.”
-
Siku ya Quds Duniani:
Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi Amani ya Dunia nzima
Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi na kuidumisha Amani ya Dunia nzima. Waislamu waishi kwa Amani, Wakristo waishi kwa Amani, na hata Mayahudi waishi kwa Amani, na mtu yeyote asionewe na kudhulumiwa popote pale alipo Duniani.