29 Machi 2025 - 04:22
Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi Amani ya Dunia nzima

Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi na kuidumisha Amani ya Dunia nzima. Waislamu waishi kwa Amani, Wakristo waishi kwa Amani, na hata Mayahudi waishi kwa Amani, na mtu yeyote asionewe na kudhulumiwa popote pale alipo Duniani.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-bayt (a.s) - ABNA-; Waislamu na watu mbalimbali nchini Tanzania wamejitokeza kwa wingi kushirikia katika Maandamano ya Amani ya Siku ya Kimataifa ya Quds, yaliyofanyika leo hii (Ijumaa 28 Machi, 2025) katika Jiji la Dar-es-Salam - Tanzania kuanzia Ilala Boma, hadi katika Viwanja vya Pipo.

Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi Amani ya Dunia nzima

Maulana Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C), akiongea na vyombo vya Habari juu ya madhumuni na makusudio ya Siku ya ya Quds Duniani, amefafanua juu ya umuhimu wa Siku hii Kitaifa na Kimataifa. Kwa upande wa Kimataifa amesema: Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi na kuidumisha Amani ya Dunia nzima. Kwa maana kwamba: Waislamu waishi kwa Amani, Wakristo waishi kwa Amani, na hata Mayahudi nao waishi kwa Amani, na mtu yeyote asionewe na kudhulumiwa haki yake popote pale alipo Duniani. Amani ya Palestina, ni sababu ya Amani na Utulivu wa Dunia nzima.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha