2 Oktoba 2025 - 17:46
Ukimya wa Kifo wa Nchi za Kiislamu; Asia ya Magharibi, “Palestina Mpya”

Kukubaliana kwa baadhi ya nchi za Kiislamu na mpango wa kinachoitwa mpango wa amani wa Trump kuhusu Palestina, ni alama ya aibu juu ya ulimwengu wa Kiislamu na baadhi ya viongozi wao wasio na imani ya kweli, na aibu hii haitafutika hadi Siku ya Kiyama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari ya Ahlul-Bayt(a.s) -ABNA-: Kauli za Donald Trump, Rais wa zamani wa Marekani, kuhusu ndoto yake ya “Palestina Mpya” endapo atarejea madarakani, zimeibua mijadala mikubwa ya kimataifa. Trump ameitaja Palestina mpya kwa maneno ya “mchanga, bahari na jua” akidai kuwa itakuwa kituo cha utalii na maisha ya anasa yanayofanana na Lebanon ya zamani.

Hata hivyo, wachambuzi wanasema wazi kwamba Trump atabaki kimya kuhusu “operesheni za usafishaji” za Israel katika eneo hilo, jambo linaloonyesha wazi kuwa mpango huu ni wa Kizayuni. Palestina mpya inayodaiwa kuundwa kwa msaada wa Israel, itakuwa ni ardhi ambayo Wapalestina watakuwa wameshafutwa kabisa, na badala yake kutaundwa jamii bandia iitwayo “Wayahudi wa Kipalestina”.

Kwa hakika, mradi huu wa Kizayuni unalenga kuunda “taifa jipya” Mashariki ya Kati, na kufufua Ufalme Mkubwa wa Kiyahudi kupitia makundi kama vile Wayahudi Wakurdi, Waarabu, Alawiyyah, Waturuki na hatimaye “Wayahudi wa Palestina.”

Mpango huu unalindwa na sera ya usafishaji wa kikabila iliyotekelezwa hatua kwa hatua kwa zaidi ya miaka 70. Mchakato ulioanza na vita vya Ghuba ulifuatiwa na kuondolewa kwa viongozi wenye nguvu katika nchi zao kwa mikono ya “watekaji na wauaji” waliotumwa.

Cha ajabu, nchi kadhaa za Ulaya zimejitokeza kutangaza kutambua Palestina kama taifa. Lakini swali kubwa ni: ni ipi Palestina inayotambuliwa? Palestina mpya iliyoundwa na Israel huku watu wake wa asili wakifutwa kabisa?

Wazi ni kuwa Palestina mpya itaundwa na wale wanaoitwa Wayahudi wa Palestina. Hii ni njama ya wazi ya Kizayuni ya kutengeneza taifa jipya Mashariki ya Kati lenye asili ya Kiyahudi.

Aidha, harakati za Kizayuni barani Ulaya haziwezi kupuuzwa. Hivi karibuni wameanzisha mashirika yenye majina ya kudanganya kama Shirikisho la Alawiyyah wa Kiarabu Ulaya, jumuiya ya Wakurdi nchini Ujerumani na muungano unaoitwa Alawiyyah-Kurdi. Vyombo hivi vipya vinapewa kipaumbele na kuungwa mkono, hasa vile vinavyoendeshwa kwa mtazamo wa kisekula na kimaisha.

Hitimisho:
Nchi za eneo hili hususan ulimwengu wa Kiislamu zinapaswa kumaliza ukimya na kutojali. Hawapaswi kuruhusu mapambano ya Palestina ambayo yamedumu kwa damu na roho za maelfu ya mashahidi wa Kiislamu kupotezwa. Ukimya huu ni sawa na kuiweka dini ya Uislamu na Waislamu katika giza kamili.

Kukubaliana kwa baadhi ya nchi za Kiislamu na mpango wa kinachoitwa amani ya Trump kuhusu Palestina, ni alama ya aibu isiyofutika juu ya ulimwengu wa Kiislamu na baadhi ya viongozi wasio na imani ya kweli, na doa hili halitafutika hadi Siku ya Kiyama.

Kwa masikitiko, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi nane ikiwemo Uturuki, Jordan, Umoja wa Falme za Kiarabu, Indonesia, Pakistan, Saudi Arabia, Qatar na Misri, walitoa taarifa ya pamoja baada ya kutangazwa kwa pendekezo la Trump la vipengele 20 vya kumaliza vita vya Gaza, wakilikaribisha pendekezo hilo.

Katika taarifa hiyo, walisema:
“Tunakaribisha uongozi na juhudi za dhati za Trump kwa ajili ya kumaliza vita vya Gaza; tunasisitiza umuhimu wa kushirikiana na Washington katika kusimamia amani ya eneo.”

Mawaziri hao waliongeza kuwa wako tayari kushirikiana kwa njia chanya na ya kujenga na Marekani pamoja na wadau husika kwa ajili ya kuhitimisha na kutekeleza makubaliano hayo, ili kuhakikisha amani, usalama na uthabiti wa eneo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mpango huu unajumuisha:

1- Kuwasilishwa kwa msaada wa kibinadamu bila vikwazo kwa Gaza,

2- Kuzuia kufukuzwa kwa Wapalestina,

3- Kuachiliwa kwa mateka,

4- Kuunda mfumo wa usalama kwa ajili ya pande zote,

5- Kuondoka kabisa kwa Israel,

6- Ukarabati wa Gaza, na

7- Kuweka njia ya suluhisho la mataifa mawili kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Masharti haya yametajwa kuwa muhimu kwa uthabiti na usalama wa eneo.

Mwandishi: Dkt. Hassan Sadeghian - mchambuzi wa siasa za Uturuki na Kaukazi

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha