Asia
-
Iran Yaeleza Mkutano wa Usalama wa Marekani na Nchi za Kanda ni Maonyesho ya Kisiasa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amesema mkutano wa kile kilichoitwa "Mazungumzo ya Usalama wa Kikanda" ulioandaliwa na Marekani nchini Bahrain ni wa maonyesho tu na unalenga kuficha sera ambazo, kwa mujibu wake, zinachochea ukosefu wa utulivu katika eneo la Asia Magharibi.
-
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Karate ya Iran Yatwaa Dhahabu ya Asia
Timu ya taifa ya wanawake ya karate ya Iran imeibuka bingwa wa Mashindano ya Karate ya Asia baada ya kuifunga Japan katika fainali na kutwaa medali ya dhahabu.
-
Wazayuni Wajibu Kauli za Trump: “Sisi Hatuko Chini ya Utawala wa Marekani!”
Hali ya sasa ya utawala wa Kizayuni (Israel) kutokana na utegemezi wake mkubwa kwa siasa za Marekani pamoja na changamoto za ndani, imegeuka kuwa moja ya hatua muhimu za kihistoria katika uhusiano wa kimataifa wa utawala huo. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha mabadiliko ya kimkakati katika siasa za Israel na namna inavyoshirikiana na jamii ya kimataifa na Wapalestina.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amwambia Rais wa Marekani:
“Wewe ni nani hasa?”
Khamenei: "Rais wa Marekani alisafiri hadi Palestina iliyokaliwa kwa mabavu na kutoa maneno matupu yenye kejeli ili kuwatia moyo Wazayuni waliokata tamaa."
-
Kumbukumbu Maalum:
Ukimya wa Kifo wa Nchi za Kiislamu; Asia ya Magharibi, “Palestina Mpya”
Kukubaliana kwa baadhi ya nchi za Kiislamu na mpango wa kinachoitwa mpango wa amani wa Trump kuhusu Palestina, ni alama ya aibu juu ya ulimwengu wa Kiislamu na baadhi ya viongozi wao wasio na imani ya kweli, na aibu hii haitafutika hadi Siku ya Kiyama.
-
Mazoezi ni Afya: Jamiat Al-Mustafa (s) Yaendeleza Michezo kwa Ajili ya Kuimarisha Afya ya Mwili na Akili
Kwa hakika, michezo na mazoezi haya yamekuwa kielelezo cha namna Uislamu unavyopenda mwili wenye nguvu, akili timamu, na mshikamano wa kijamii, ili kumsaidia Muislamu kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya kidini, kijamii na kiulimwengu.
-
Makala Maalum | Uso Halisi wa Marekani – Donald Trump Afichua Uso wa Kweli wa Marekani - Sura ya Ubeberu Bila Kivuli!
Donald Trump kama Mwakilishi wa Wazi wa Utawala wa Marekani, Afichua Uso Halisi wa Taifa Hilo Donald Trump, aliyekuwa rais wa Marekani, alijitokeza kama mwakilishi wa bila kificho wa watawala wa Marekani, na kupitia matendo yake, aliweka wazi sura halisi ya historia na utambulisho wa nchi hiyo. Kwa hatua yake ya kubadili jina la "Wizara ya Ulinzi" kuwa "Wizara ya Vita", Trump alifichua ukweli kwamba Marekani haiko tena tayari kujificha nyuma ya maneno ya "ulinzi" na "usalama wa kimataifa". Badala yake, alionyesha kuwa taifa hilo sasa linataka kujenga dunia mpya inayozingatia sheria ya vita, si sheria za haki za binadamu au amani ya kimataifa.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ataka Utekelezaji wa Makubaliano ya Kistratejia kati ya Iran na China
Ayatollah Khamenei amesisitiza nafasi ya kihistoria na ya kimkakati ya Iran na China katika bara la Asia na duniani, na akasema kuwa: "Iran na China, zikiwa na historia ya ustaarabu wa kale katika pande mbili za Asia, zina uwezo wa kuleta mabadiliko katika medani ya kimataifa na kikanda. Kuweka katika vitendo vipengele vyote vya makubaliano ya kistratejia, kutarahisisha njia hii."