Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (as) -ABNA- Donald Trump anaweza kuelezewa kama sura isiyo na vipodozi ya watawala wa Marekani. Wakati marais waliomtangulia walijitahidi kuonyesha taswira ya Marekani kama taifa la kidemokrasia, la amani na ustaarabu, Trump alifunua asili halisi ya Taifa hilo - Asili ya uhalifu, ubaguzi na mabaki ya wahalifu wa Ulaya waliotupwa barani Amerika.
Kwa hatua ya kubadilisha jina la “Wizara ya Ulinzi” kuwa “Wizara ya Vita”, Trump alitoa ujumbe wa wazi kwa dunia: Marekani haina tena haja ya kujificha nyuma ya sura ya polisi mwema wa dunia.
Kwa hakika, kama historia inavyothibitisha, Marekani haijawahi kuwa na wizara ya kweli ya ulinzi. Tangu kuanzishwa kwake, imekuwa ikiongozwa na mantiki ya vita, lakini ilificha ukweli huo nyuma ya maneno matamu ya kisiasa. Trump alivua pazia hili.
Ujumbe wake kwa dunia ya leo – dunia inayozungumza kwa ngumi na risasi – ulikuwa: “Either you are with us, or under our boots” / (Ama uko nasi, au uko chini ya buti zetu!)
Hatua hiyo ilionyesha pia ubatili wa taasisi za kimataifa, kuanzia Umoja wa Mataifa hadi mashirika ya kutetea haki za binadamu, ambazo zimenyamaza kimya mbele ya mauaji ya wanawake na watoto wa Kipalestina, kwa sababu tu hawakutaka kuondoka kwenye ardhi ya mababu zao.
Trump aliweka wazi kuwa sheria mpya ya dunia ni vita, sio haki, sio maadili ya kibinadamu. Hii ni kurudi kwa enzi za ubeberu, lakini sasa kwa kutumia makombora ya kisasa, ndege za kivita zisizoonekana na majeshi ya kimtandao (cyber armies).
Kwa kusema kweli, kile alichofanya Trump ni kuondoa unafiki wa Marekani na kuonyesha sura yake halisi:
-
Taifa lililojengwa juu ya mauaji ya Wenyeji Wekundu (Red Indians)
-
Na lililotumia damu ya watumwa kutoka Afrika kuendeleza uchumi wake
Kwa kuangalia kwa kina, hii pia inaweza kuwa ishara ya mwisho wa enzi ya ubeberu wa Marekani – na mwanzo wa kuporomoka kwake.
Ujumbe kwa mataifa huru na watu wenye utu ni wazi:
Wakati Marekani ikifichua sura yake ya kweli, umuhimu wa mshikamano, kujitegemea na kusimama dhidi ya dhulma unakuwa mkubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
Your Comment