Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Uislamu, mbali na kuhimiza ibada za kiroho, pia umeweka msisitizo mkubwa juu ya umuhimu wa kuimarisha afya ya mwili na akili. Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Maimamu watoharifu (a.s) wamefundisha kuwa muumini mwenye nguvu ni bora kuliko muumini dhaifu, kwani afya njema ni nguzo ya kutekeleza ibada na majukumu ya kijamii kwa ufanisi.
Kwa kuzingatia ukweli huu, Chuo cha Jamiat Al-Mustafa (s) Dar es Salaam, Tanzania, kimeweka utaratibu wa mara kwa mara wa kufanya mazoezi ya kiafya kupitia mchezo wa mpira wa miguu. Shughuli hizo hufanyika katika Kiwanja cha Salon, kilichopo Kigamboni katika Hawza ya Mabanati wa Kiislamu ya Hazrat Zainab (s.a).
Michezo hii huwashirikisha wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa pamoja na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Bara la Asia, wakiwemo Wairan na Wafghanistani. Ushiriki huo si wa kijamii pekee bali pia unaleta mshikamano wa Kiislamu, mshikikano wa kijamii na kuimarisha undugu miongoni mwa Waislamu wa mataifa tofauti.
Kwa hakika, michezo na mazoezi haya yamekuwa kielelezo cha namna Uislamu unavyopenda mwili wenye nguvu, akili timamu, na mshikamano wa kijamii, ili kumsaidia Muislamu kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya kidini, kijamii na kiulimwengu.
Your Comment