Akinukuu Aya ya 108 ya Surah Yusuf, Sheikh Ghawth alisisitiza umuhimu wa kutumia akili, mazingatio na dalili za ulimwengu wa nje (Ulimwengu wa Dhahiri) katika kumuelewa Muumba.
Katika majlisi ya maombolezo ya kuadhimisha shahada ya Imamu Jawad (a.s) iliyofanyika katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, Ayatollah Reza Ramadhani — Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s) — alisisitiza: "Kufaidika na mafundisho na maneno ya Ahlul Bayt (a.s) hutusaidia katika safari ya kimatendo ya kumkaribia Mwenyezi Mungu." Amebainisha kuwa: "Maudhui yanayotolewa na Ahlul Bayt (a.s) ni ya ki-Tawhidi, yamejengwa juu ya msingi wa maumbile ya mwanadamu (fitra), na yanakubaliana kikamilifu na akili ya binadamu."