9 Desemba 2025 - 14:28
Afisa wa Jeshi la Israel: Theluthi Moja ya Wanajeshi Wanakabiliwa na Matatizo ya Akili

Ripoti rasmi za utawala wa Kizayuni zinaonyesha kuongezeka kwa kiwango kisicho cha kawaida cha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa wanajeshi. Kwa mujibu wa Tamar Shimony, Naibu Mkuu wa Idara ya Urejeshaji (Rehabilitation) katika Wizara ya Vita ya Israel, zaidi ya wanajeshi 85,000 wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kisaikolojia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s)  -ABNA- takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya wanajeshi 85,000 wa Israel tangu kuanza kwa vita ya kinyama dhidi ya Gaza wanaishi na matatizo makali ya kiakili. Hili ni ongezeko kubwa lisilokuwa na mfano katika miaka ya karibu.

Mnamo tarehe 7 Oktoba 2023, idadi ya wanajeshi waliokuwa wakipokea matibabu ya kisaikolojia ilitangazwa kuwa 62,000—ikionyesha ongezeko kubwa la wagonjwa wapya baada ya vita kuendelea.

Theluthi Moja ya Wanajeshi Waathirika

Tamar Shimony ameeleza kuwa:

  • 1-Takribani asilimia 33 (theluthi moja) ya wanajeshi wamepata matatizo ya akili yanayohusishwa na mashambulizi na mapigano baada ya Operesheni “Tufani ya Al-Aqsa”.
  • 2-Madaktari wa kisaikolojia sasa wanalazimika kuhudumia hadi wagonjwa 750 kila mmoja, jambo linalofanya matibabu yawe duni na yasiyofikia viwango vinavyotakiwa.

Mgogoro wa Afya ya Akili Katika Jamii ya Kizayuni

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa mgogoro huo hauko jeshini pekee:

  • 1-Gazeti Yedioth Ahronoth linaripoti kuwa takribani Wayahudi Wazayuni milioni 2 wanahitaji huduma za afya ya akili kwa kiwango fulani.
  • 2-Ripoti pia zinaonyesha kuongezeka kwa matukio ya kujiua miongoni mwa wanajeshi, ikiwa ni pamoja na vifo vya wanajeshi wawili wiki iliyopita vilivyosababishwa na msongo na athari za kiakili za vita.

Matukio ya Kujiua Yameongezeka

Kwa mujibu wa takwimu rasmi:

  • 1-Matukio 279 ya kujaribu kujiua yameripotiwa katika kipindi cha miezi 18,
  • 2-Ambapo 36 kati ya hayo yamesababisha vifo.

Sababu Kuu: Vita vya Kinyama Gaza

Wataalamu wa masuala ya kijamii na kisaikolojia wanasema kuwa:

  • 1-Kuendelea kwa vita katili dhidi ya Gaza,
  • 2-Na mauaji ya zaidi ya Wapalestina 70,000,

kumekuwa na athari kubwa si tu kwa Wapalestina, bali pia kumefanya jeshi na jamii ya Israel kukumbwa na msongo mkubwa wa kisaikolojia, kuharibika kwa hali ya kijamii, na kuongezeka kwa magonjwa ya akili.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha