wanajeshi
-
Washington Post: Idadi halisi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa katika vita na Iran ni kubwa kuliko ilivyoripotiwa na Pentagon
Maafisa wenye taarifa kuhusu idadi kubwa zaidi ya vifo wameeleza wasiwasi wao kuhusu kutorekodiwa kwa baadhi ya vifo hivyo katika hifadhidata ya umma ya Pentagon. Wizara ya Vita ya Marekani pia imekataa kujibu maswali ya Washington Post kuhusu sababu ya tofauti hiyo.
-
Iran Yaionya Marekani: Ikiwa Mzingiro wa Baharini Utaendelea, Jeshi la lran Litafanya Mashambulizi Makali Zaidi Dhidi ya Meli za Kijeshi za Marekani
Msemaji wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (saww) ya Iran ameionya Marekani kwamba endapo itaendelea kuzuia na kusumbua meli za Iran baharini, Jeshi la Wanajeshi la Iran litazidisha mashambulizi makali zaidi dhidi ya meli za kijeshi za Marekani katika eneo hilo.
-
Msemaji wa Jeshi la Iran: Jeshi la Marekani Limepoteza Ari na Nguvu ya Kupambana
Msemaji wa Jeshi la Iran amesema wanajeshi wa Marekani walioko Mashariki ya Kati wamekumbwa na hali ya kukata tamaa na kupoteza ari, akisisitiza kuwa jeshi linalokosa utashi na imani haliwezi kushinda katika uwanja wa vita.
-
Mashambulizi ya Saudi Arabia na Marekani dhidi ya Hashd al-Shaabi Yazua Maswali Kufuatia Ziara ya Waziri Mkuu wa Iraq Marekani
Mashambulizi yaliyotekelezwa na Saudi Arabia na Marekani dhidi ya vituo vya Hashd al-Shaabi yamesababisha vifo vya zaidi ya wanajeshi 20 wa Iraq, huku yakizua mjadala kuhusu matokeo ya ziara ya Waziri Mkuu mpya wa Iraq nchini Marekani na mkutano wake na Rais wa Marekani, Donald Trump.
-
Walioleta Kambi za Marekani Kuzunguka Iran Leo Wanalia: Kwa Nini Iran Inatushambulia?
Kwa miaka mingi, Iran iliwaonya majirani zake wa Kiarabu kuhusu hatari ya kuruhusu Marekani kujenga kambi za kijeshi katika ardhi zao, ikisema uwepo wa majeshi ya kigeni ungeweza kuzifanya nchi hizo kuwa sehemu ya vita dhidi ya Iran. Leo, baada ya kuanza kwa mapambano, kambi hizo zimegeuka kuwa maeneo ya mashambulizi, huku watawala wa Kiarabu wakijikuta wakikabiliwa na matokeo ya maamuzi waliyoyafanya hapo awali.
-
Walinzi wa Mapinduzi wa Iran Wawashukuru Wananchi wa Jordan na Kutangaza Kulenga Ndege za Marekani Katika Uwanja wa Ndege wa Aqaba
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran wamewashukuru wananchi na wanajeshi wa Jordan kwa taarifa walizodai zilisaidia katika mashambulizi dhidi ya vituo vya Marekani, huku wakitangaza kulenga ndege za kijeshi za Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Aqaba.
-
IRGC yadai kushambulia vituo vya kimkakati vya Marekani nchini Jordan kwa makombora ya balestiki
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuwa katika awamu ya tatu ya wimbi la pili la Operesheni "Nasr-2" lililenga vituo vya kimkakati na maeneo ya wanajeshi wa Marekani katika kambi ya anga nchini Jordan kwa kutumia makombora ya balestiki.
-
IRGC yatangaza awamu ya pili ya Operesheni "Nasr 2"; yadokeza kushambulia vituo vya mawasiliano na makazi ya wanajeshi wa Marekani Bahrain
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuwa katika awamu ya pili ya Operesheni "Nasr 2" lililenga maghala ya silaha, kituo cha mawasiliano ya satelaiti na jengo la makazi ya wanajeshi wa Marekani katika Kambi ya Al-Juffair nchini Bahrain.
-
Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa: Adui Hana Njia Nyingine Isipokuwa Kukubali Kushindwa na Kusalimu Amri
Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa (as) yamesema wananchi wa Iran na vikosi vyao vya ulinzi, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na chini ya uongozi wa Amiri Jeshi Mkuu, vimethibitisha kuwa Marekani na Israel hawana njia nyingine isipokuwa kukiri kushindwa na kusalimu amri mbele ya uthabiti wa taifa la Iran.
-
Ripoti ya Channel 13: Israel Yaendelea Kupata Hasara Lebanon Bila Lengo la Wazi la Kijeshi
Televisheni ya Channel 13 ya Israel imeripoti kuwa jeshi la Israel linaendelea kupata hasara dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon, huku changamoto za kijiografia na mgogoro wa kisiasa vikizidisha hali ngumu ya operesheni hiyo.
-
Mexico Bado Katika Ghasia; Wanajeshi 25 wa Walinzi wa Taifa Wauawa
Machafuko nchini Mexico yanaendelea kufuatia kifo cha kiongozi wa moja ya karteli hatari, huku wanajeshi 25 wa Walinzi wa Taifa wakiripotiwa kuuawa katika wimbi la vurugu.
-
Afisa wa Jeshi la Israel: Theluthi Moja ya Wanajeshi Wanakabiliwa na Matatizo ya Akili
Ripoti rasmi za utawala wa Kizayuni zinaonyesha kuongezeka kwa kiwango kisicho cha kawaida cha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa wanajeshi. Kwa mujibu wa Tamar Shimony, Naibu Mkuu wa Idara ya Urejeshaji (Rehabilitation) katika Wizara ya Vita ya Israel, zaidi ya wanajeshi 85,000 wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kisaikolojia.
-
Mwisho mchungu wa ushirikiano wa askari wa Afghanistan na serikali ya Marekani
Wanajeshi wa zamani wa Afghanistan ambao walikuwa wakishirikiana na shirika la ujasusi la Marekani, baada ya miaka mingi ya huduma, sasa wanakabiliwa na matatizo makubwa wakiwa nchini Marekani.
-
Mgogoro usio wa kawaida katika Jeshi la Israel / Kupungua kwa kasi kwa hamasa ya wanajeshi kuendelea na utumishi
Jeshi la utawala wa Kizayuni linakabiliwa na mgogoro usio wa kawaida wa upungufu wa askari na kushuka kwa kiwango kikubwa cha hamasa ya wanajeshi kuendelea na utumishi.
-
Kifo cha Kishahidi Klcha Kijana Msyria Usiku wa Harusi Yake Akiwa Anapambana na Uvamizi wa Israel katika Mji wa Bayt Jinn
Kijana mmoja Msyria ameuliwa shahid usiku wa harusi yake wakati akipambana na uvamizi wa jeshi la Israel katika mji wa Bayt Jinn, ulioko katika vitongoji vya kusini mwa Damascus.
-
Wanajeshi 11 wa Usalama wa Pakistan Wauawa Kwenye Mpaka wa Afghanistan
Baada ya shambulio la silaha karibu na mpaka wa Afghanistan, wanajeshi 11 wa Pakistan waliuawa.