Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Kutokana na maafisa wa juu wa jeshi la utawala wa Kizayuni kutoa onyo la mara kwa mara kuhusu ongezeko la upungufu wa askari, utafiti mpya umeonyesha kuwa jeshi hilo limeingia katika mgogoro mkubwa na usio na kifani wa kuhifadhi na kudumisha askari wake.
Kulingana na televisheni ya Channel 12, jeshi la Israeli linakabiliwa na upungufu wa takribani maafisa 1,300 katika vyeo vya Luteni na Kapteni, pamoja na upungufu wa karibu maafisa 300 katika cheo cha Meja.
Kwa mujibu wa tafiti za ndani ya jeshi, ni asilimia 63 tu ya maafisa wanaotaka kuendelea na utumishi, ilhali mwaka 2018 kiwango hicho kilikuwa asilimia 83. Miongoni mwa askari wasio maafisa (degederedari), utayari wa kuendelea na huduma umeshuka kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi asilimia 37 mwaka huu.
Kwa miaka mingi, jeshi la Israeli limekuwa na changamoto ya kuhifadhi askari wa kudumu, kwani kazi katika sekta ya kiraia imekuwa ikionekana kuwa na maslahi makubwa ya kifedha na kuwapa watu majukumu machache na maisha yenye utulivu zaidi.
Mgogoro wa sasa umezidishwa na:
-
Uchovu uliosababishwa na vita,
-
Mazingira magumu ya utumishi,
-
Mvutano wa kisiasa ndani ya utawala,
-
Na hali ya kutoridhishwa kwa askari kuhusu uteuzi wa hivi karibuni wa makamanda wakuu wa jeshi.
Mnamo Novemba uliopita, maafisa wakuu wa Idara ya Rasilimali Watu ya jeshi waliiambia Kamati ya Knesset kuwa karibu askari 600 wa kikosi cha kudumu wameomba kustaafu mapema, na maafisa wachanga wanapandishwa vyeo kabla ya muda ili kuziba mapengo.
Mkuu wa Majeshi (Chief of Staff) na Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu — sambamba na viongozi wengine wa utawala — wako katika hatua za kutengeneza mipango ya kukabiliana na mgogoro huu na kuzuia kupitishwa kwa sheria mpya ambazo zinaweza kuzidisha hali ya askari wa kudumu.
Kwa sasa, karibu vijana wa Haredi 80,000 wenye umri wa miaka 18–24 wanaostahili kujiunga na jeshi hawajajiandikisha. Kwa upande mwingine, jeshi la Israeli linasema linahitaji haraka askari 12,000 wapya ili kupunguza mzigo mzito uliosababishwa na vita dhidi ya Hamas huko Gaza na changamoto nyingine za kijeshi.
Your Comment