Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuongezeka kwa pengo la imani anayokabiliana nalo Donald Trump ndani na nje ya Marekani, huku sera yake ya makabiliano na kuongezeka kwa mivutano ikianza kuchunguzwa zaidi na kusababisha mpasuko katika msingi wa wafuasi uliomfikisha Ikulu ya White House.
Wakati Donald Trump alipodai Jumatatu kuwa ameweka rekodi mpya ya umaarufu wake, matokeo ya kura za maoni zinaonyesha kuwa Wamarekani wengi hawaridhiki na utendaji wake, hasa katika masuala ya uchumi na uhamiaji.
Jeshi la utawala wa Kizayuni linakabiliwa na mgogoro usio wa kawaida wa upungufu wa askari na kushuka kwa kiwango kikubwa cha hamasa ya wanajeshi kuendelea na utumishi.