5 Februari 2026 - 11:24
Kura za maoni zapinga madai ya Trump; Wamarekani wengi hawaridhiki na utendaji wa rais

Wakati Donald Trump alipodai Jumatatu kuwa ameweka rekodi mpya ya umaarufu wake, matokeo ya kura za maoni zinaonyesha kuwa Wamarekani wengi hawaridhiki na utendaji wake, hasa katika masuala ya uchumi na uhamiaji.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- licha ya Donald Trump, rais wa Marekani, kudai kuwa ana kiwango cha juu zaidi cha umaarufu wake, tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa kuridhika kwa umma kuhusu utendaji wake, hasa katika sekta ya uchumi na uhamiaji, kumeendelea kushuka na kusababisha kutoridhika kwa wananchi wengi wa Marekani.

Trump aliandika mwishoni mwa Jumatatu kwenye mtandao wa kijamii wa “Truth Social” akidai kuwa umaarufu wake uko “juu kuliko wakati wowote”, na kusema kuwa wapiga kura wanataka “nchi imara yenye uchumi bora zaidi katika historia”. Madai hayo yanapingwa na takwimu za kura za maoni zilizochapishwa wiki za karibuni, zinazoonyesha tofauti kubwa kati ya simulizi la rais wa Marekani na hali halisi ya maoni ya umma.
Kutoridhika kwa ujumla na utendaji wa Trump
Kwa mujibu wa kura ya pamoja ya jarida la The Economist na taasisi ya YouGov, asilimia 54 ya Wamarekani hawaidhinishi utendaji wa jumla wa Trump. Ingawa Trump bado anaungwa mkono sana na Warepublican, ambapo asilimia 86 yao wanaridhika naye, upinzani mkali wa watu huru (independents) na Wademocrat umepelekea kushuka kwa umaarufu wake kitaifa.

Uchumi; kisiki cha serikali ya Marekani

Uchumi umekuwa mojawapo ya sababu kuu za kutoridhika kwa umma dhidi ya serikali ya Trump. Kwa mujibu wa kura hiyo hiyo, asilimia 53 ya raia wa Marekani hawaridhiki na namna rais anavyoendesha uchumi, na ni asilimia 39 tu wanaounga mkono sera zake.

Kura ya Associated Press na taasisi ya NORC iliyofanywa mapema Januari pia inaonyesha kuwa karibu asilimia 60 ya waliohojiwa hawaridhiki na utendaji wa jumla wa Trump.

Ingawa kiwango cha mfumuko wa bei Marekani Desemba 2025 kilifikia asilimia 2.7, kuongezeka kwa gharama za maisha kumeongeza mzigo kwa familia. Takwimu za Ofisi ya Takwimu za Kazi ya Marekani zinaonyesha kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, ikiwemo:
ongezeko la 18.7% la bei ya kahawa iliyooka, na ongezeko la 15.5% la bei ya nyama ya kusaga ikilinganishwa na mwaka uliopita.
 

Uhamiaji na usalama; sababu ya kushuka zaidi kwa umaarufu
Matokeo ya kura ya Reuters/Ipsos yanatoa taswira mbaya zaidi ya umaarufu wa Trump, ambapo kiwango cha kuridhika na utendaji wake kimeshuka hadi asilimia 38, kiwango cha chini zaidi katika muhula wake wa pili wa urais. Katika kura hiyo, asilimia 53 ya washiriki walionyesha kutoridhishwa na sera zake za uhamiaji.

Kushuka huku kumetokea baada ya kuongezeka kwa ukosoaji dhidi ya hatua kali za serikali ya shirikisho kuhusu wahamiaji, hasa baada ya operesheni tata za majeshi ya shirikisho katika jimbo la Minnesota na matukio ya ufyatuaji risasi yaliyoua watu huko Minneapolis, yaliyopata uangalizi mkubwa wa vyombo vya habari vya Marekani.

Marekani katika mtazamo wa wapiga kura iko kwenye mwelekeo wa kudorora
Kura ya New York Times na Siena College iliyofanywa katikati ya Januari inaonyesha kuwa sehemu kubwa ya wapiga kura wa Marekani wanaamini Trump katika mwaka wa kwanza wa muhula wake wa pili amejikita kwenye vipaumbele visivyo sahihi.
Kwa mujibu wa kura hiyo, ni asilimia 32 tu walisema hali ya nchi imeimarika, huku asilimia 49 wakisema hali ya Marekani imekuwa mbaya zaidi.

Kura hiyo pia inaonyesha mgawanyiko mkubwa wa kisiasa katika jamii ya Marekani, ambapo asilimia 42 ya raia wanaona Trump anaelekea kuwa miongoni mwa marais wabaya zaidi katika historia ya Marekani, na ni asilimia 19 tu wanaotarajia awe miongoni mwa bora zaidi - takwimu zinazoonyesha kuendelea kwa mgogoro wa imani ya umma katika mfumo wa kisiasa wa Marekani.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha