Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jeshi la Israel linapanga kuwalenga zaidi Wayahudi vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 25 kutoka Marekani na Ufaransa, kuwahimiza wahamie katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kujiandikisha jeshini kwa kipindi cha miaka kadhaa.
Kitengo cha wanawake cha Umoja wa Mataifa, katika kuelekea kumbukumbu ya miaka minne tangu Taliban ichukue madaraka nchini Afghanistan, kimetoa taarifa ikikosoa vikali mwenendo wa kundi hilo kuhusu wanawake wa Afghanistan.
Akielezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kibinadamu huko Gaza, Papa Francis amesisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kukabiliana na mgogoro huu na kusaidia watu wasio na hatia.