Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Meja Jenerali Mohammad Pakpour, amesisitiza kuwa wanajeshi wa Jeshi la Iran (IRGC) wako tayari kurudia mashambulizi makali dhidi ya maadui.
Akizungumza wakati wa kikao chake na Kamanda wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Hatami, alisema kwa msisitizo: "Hatutaacha Maadui Wavamizi (na Wachokozi), vita na mapambano dhidi ya adui yataanzia katika nukta ile tulipoishia."
Katika hotuba yake, Jenerali Pakpour aliwahimiza wanajeshi kwa kutaja hadhi ya mashujaa waliouawa, akiwemo Luteni Jenerali Shahidi Mohammad Bagheri, Shahidi Hussein Salami, Shahidi Gholam Ali Rashid, na Shahidi Ali Shadmani.
Aliisifu ari ya mapambano ya wananchi wa Iran katika utetezi wa heshima uliodumu kwa siku 12, akisema kuwa mshikamano wa wananchi ndio nguvu kuu ya majeshi ya Iran. Alisisitiza kuwa: “Umoja katika wingi” ndio ngome imara zaidi ya Iran, ambayo imeweza kushinda njama hatari zaidi katika historia kwa msaada wa kishujaa kutoka kwa wananchi.
Jenerali Pakpour alisisitiza kuwa majeshi ya Iran yako katika hali ya juu ya utayari na mshikamano kamili kurudia mashambulizi dhidi ya adui, akibainisha kuwa: “Waisraeli wameuona moto wa kuzimu walioahidiwa kwa macho yao wenyewe katika siku za mwisho za vita.”
Kwa msimamo mkali, alionya kuwa: "Hatutaacha (maadui wachokozi na) wavamizi. Tutaendeleza vita kuanzia pale tulipoishia."
Your Comment