Wavamizi
-
Kuanza kwa kuondoka kwa majeshi ya wavamizi (wa kizayuni) kutoka Ghaza
Baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Ghaza yanashuhudia kuondoka kwa hatua kwa hatua kwa majeshi ya utawala wa Kizayuni na kuanza kwa kurejea kwa wakimbizi.
-
Katika taarifa ya pekee imesema:
"Wanaume majemedari wa Ansarullah wamewaacha Wazayuni katika wasi wasi / Taifa la Yemen linamfufua mataifa yaliyozama usingizini"
“Umma wa Malk Khashab,” Mwanahabari wa kike wa Ansarullah, aliandika: Katika mapambano kati ya wavamizi na Wazayuni dhidi ya Yemen, hesabu zote zimebadilika na mizani imegeuzwa. Kwa hivyo, walianza kulia na kupiga kelele kutokana na wanaume imara wa Yemen na wana-yemen kwa ujumla, na sasa Yemen imekuwa moto wa kuotea mbali na ndoto za kutisha kwao zinazowaamsha mara kwa mara.
-
Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu wa Bahrain:
Kujiondoa kwenye njia ya Muqawama (Mapambano ya kupinga dhulma) ni sawa na fedheha na udhalili
Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu wa Bahrain alisisitiza kuwa kuacha njia ya Muqawama (mapambano dhidi ya wavamizi na dhulma) hakuzai chochote isipokuwa fedheha, udhalilishaji na utumwa.
-
Mkuu wa Majeshi: Vikosi vya Ulinzi vya Iran Vitatoa Jibu Kali Zaidi ya Mawazo ya Wavamizi
“Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kwa mwongozo wa Kiongozi Muadhamu Ayatollah Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu amlinde), vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viko tayari kugeuza tishio lolote kuwa fursa ya kustawisha nguvu za taifa na kuinua hadhi ya Iran katika mizani ya kimkakati ya kikanda na kimataifa. Jibu letu kwa maadui litakuwa la wakati, kali, la kuumiza na zaidi ya walivyowahi kufikiria.”
-
Hezbollah: Uhalifu wa Wavamizi Dhidi ya Yemen Unaonesha Kiwango cha Kufilisika Kwao
Hezbollah imetoa tamko likisema kuwa: "Uhalifu na mashambulizi yanayofanywa na wavamizi (yaani utawala wa Kizayuni wa Israel) dhidi ya Yemen ni ishara ya wazi ya kufilisika kwao kisiasa, kiakhlaqi na kijeshi."
-
Al-Bukhaiti: "Vita imeingia katika awamu mpya na wavamizi watalipa gharama kubwa"
Mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ametangaza kuwa shambulio dhidi ya kikao cha Serikali ya Yemen huko Sana'a lilivuka mistari miekundu na kwamba vita imeingia katika awamu mpya.
-
Mufti wa Oman:
“Inasikitisha kuwa waandishi wa habari wanauawa Gaza na baadhi wanaendelea kuwaunga mkono wavamizi”
Mufti wa Oman amelaani mauaji ya waandishi wa habari katika mji wa Gaza yaliyofanywa na jeshi la Israel, na kutamka masikitiko yake juu ya kuendelea kwa baadhi ya watu na nchi kuunga mkono wavamizi.
-
Hashd ni nguzo ya hema, na Muqawama ni heshima ya Umma wa Iraq / Hatutapatanishwa na Wavamizi
Al_Walaiy: “Tunaiweka hai Gaza ndani ya nyoyo zetu na tuko tayari daima kuwasaidia.” Alieleza kuwa ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni furaha kwao, na kwamba ndugu zao wa Lebanon ni mfano wa ushindi - ushindi uliotabiriwa na Qur’an Tukufu.
-
Kamanda wa Jeshi la Iran (IRGC) Aonya: "Tutarejelea mapigano (vita) kwa kuanzia katika nukta ile tulipoishia - Hatutamuacha Adui Mchokozi!"
Jenerali Pakpour alisisitiza kuwa majeshi ya Iran yako katika hali ya juu ya utayari na mshikamano kamili kurudia mashambulizi dhidi ya adui, akibainisha kuwa: “Waisraeli wameuona moto wa kuzimu waliokuwa wameahidiwa kwa macho yao wenyewe katika siku za mwisho za vita.”