Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - The Wall Street Journal limeripoti kuwa, wanajeshi wa Kizayuni wamefanya harakati nje ya eneo la Buffer Kusini Magharibi mwa Syria na kuanza kuwatia mbaroni raia wa Syria.
Wakaazi wa Kijiji cha Hamidiyeh katika Miinuko ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu wamesisitiza kuwa, wanajeshi wa Kizayuni wameunda eneo la bafa (kizuizi) katika nchi hii na wanawazuia raia wa Syria kuingia humo.
Mbali na kuvamia ardhi ya Syria, wavamizi hawa pia huwateka nyara raia wa nchi hii. Baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad huko Syria, pamoja na mamia ya mashambulizi ya anga dhidi ya nchi hii, utawala wa Kizayuni ulikiuka makubaliano ya mwaka 1974 kwa kuvamia eneo la Buffer (Bafa) katika Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na utawala haram wa kizayuni.
Your Comment