31 Januari 2026 - 12:53
Hatua 4 za Ibada Tukufu ya Umrah

Mwongozo wa Hatua kwa Hatua za Kukamilisha Umrah kwa Imani na Utulivu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Umrah ni hija tukufu isiyo ya lazima (ni mustahabu) yenye hatua kuu nne, na kwa kawaida huchukua takribani saa 2 hadi kukamilika. Hivyo zifuatazo hapo chini ni Hatua au Ibada nne zinachukuliwa kuwa nguzo muhimu (Arkan) za Umrah; iwapo yoyote itakosekana, Umrah haitakuwa halali:

1_Ihram - Fanya ghusl, vaa mavazi sahihi, tia nia (niyyah), soma Talbiyah, na zingatia masharti ya Ihram.

2_Tawaf - Zunguka Al-Kaaba mara 7 kinyume cha saa, fanya dua, swali rakaa mbili, na kunywa maji ya Zamzam.

3_Sa‘i - Tembea kati ya Safa na Marwa mara 7, ukifanya dua; wanaume wakimbie kidogo kati ya taa za kijani.

3_Halq/Taqsir - Wanaume wananyoa au kupunguza nywele; wanawake hupunguza kiasi cha ncha ya kidole. Hapa Umrah hukamilika na masharti ya Ihram huondolewa.

Hatua 4 za Ibada Tukufu ya Umrah

Nasaha: Kuwa mvumilivu katika msongamano, kunywa maji ya kutosha, vaa viatu vizuri, na tekeleza ibada kwa utulivu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha