Leo hii katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam - Tanzania, palifanyika Kongamano Tukufu la Qur’an ambapo wanafunzi wa kike kutoka Hawzat Hazrat Zainab (sa) walishiriki kwa umahiri na adabu kubwa.
Walikuwa mfano halisi wa utekelezaji wa mafundisho bora ya Kiislamu kuhusu namna ya kujisitiri, kuishi, na kuwasilisha ujumbe wa dini kwa vitendo.
Katika zama hizi, Hijabu imelinganishwa na kutoendelea kwa jamii na inafikiriwa kuwa ni ishara ya kifungo cha wanawake. Wahubiri wengi wanafikiria kuwa ni bora kutolizungumzia jambo hili katika majlisi zao. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Inapotokea Bid’ah na Mwanachuoni asikiseme kile akijuacho (dhidi ya Bid’ah hiyo), basi (Mwanachuoni huyo) hulaaniwa na Mwenyezi Mungu, Malaika na Wanadamu.”