Sheikh alieleza mbinu za maadui na wanyonyaji, akisema hutumia kanuni potofu ya kwamba “lengo huhalalisha njia”, hivyo hutumia njia zote mbaya ili kufikia malengo yao maovu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jalsa (Kikao) cha maadili kiimefanyika Leo hii katika Shule ya Imam Al-Hadi (as) Nchini Malawi kwa ushiriki wa wanafunzi wa dini na walimu ambapo mada muhimu ya Kimaadili iliwasilishwa na Sheikh Abdulrashid Yusuf, tarehe 31/01/2026, katika eneo la musallah (Msikiti) wa shule ya Al-Hadi (as), kuanzia saa 8:30 hadi 10:00 alasiri.
Mada ya kikao ilikuwa “Kujiandaa dhidi ya maadui wa Uislamu”, ambapo mwalimu alieleza umuhimu wa Waislamu kuwa tayari dhidi ya mashambulizi ya kimada na kiroho yanayolenga Uislamu.
Sheikh Abdulrashid Yusuf, akitumia Aya za Qur’ani Tukufu, alisisitiza kuwa Muislamu anatakiwa awe na maandalizi kamili dhidi ya maadui wa Uislamu kwa sababu hilo ni agizo la Mwenyezi Mungu. Aliongeza kuwa leo mfano wa Uislamu halisi unaonekana kwa taifa la Iran, na kwamba uadui dhidi ya taifa hilo ni uadui dhidi ya Uislamu. Iran, kwa kufuata Qur’ani na kutumia vipaji vyake, inajilinda na kusimama kwa heshima mbele ya maadui wa Uislamu.
Aidha, alieleza mbinu za maadui na wanyonyaji, akisema hutumia kanuni potofu ya kwamba “lengo huhalalisha njia”, hivyo hutumia njia zote mbaya ili kufikia malengo yao maovu.
Mwisho, aliwahimiza wanafunzi kuwa wawe macho, wachunguze kwa makini harakati za adui, ili wasiangukie mitego na hila zao.
Kikao hicho kilitoa elimu, hamasa, na kuongeza uelewa wa kidini kwa washiriki.
Your Comment