Msemaji wa Jeshi la Iran amesema kuwa vikosi vya nchi hiyo vinatumia kipindi cha usitishaji mapigano kuimarisha uwezo wake wa kivita, akisisitiza kwamba Iran itajibu kwa uthabiti dhidi ya kosa lolote litakalofanywa na adui. Pia alieleza kuwa mzozo kati ya Iran na Israel ni wa kimkakati na wa kuamua mustakabali wa pande hizo mbili.
Ripoti rasmi za utawala wa Kizayuni zinaonyesha kuongezeka kwa kiwango kisicho cha kawaida cha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa wanajeshi. Kwa mujibu wa Tamar Shimony, Naibu Mkuu wa Idara ya Urejeshaji (Rehabilitation) katika Wizara ya Vita ya Israel, zaidi ya wanajeshi 85,000 wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kisaikolojia.