Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-
Tehran - Katika kuelekea ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini China, Ofisi ya Hifadhi na Uenezi wa Maandiko ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Ayatollah Sayyid Ali Khamenei) imechapisha sehemu ya matamshi ya Kiongozi huyo kuhusu umuhimu wa mahusiano ya Iran na China kwa lugha ya Kichina katika mitandao rasmi ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ayatollah Khamenei amesisitiza nafasi ya kihistoria na ya kimkakati ya Iran na China katika bara la Asia na duniani, na akasema kuwa:
"Iran na China, zikiwa na historia ya ustaarabu wa kale katika pande mbili za Asia, zina uwezo wa kuleta mabadiliko katika medani ya kimataifa na kikanda. Kuweka katika vitendo vipengele vyote vya makubaliano ya kistratejia, kutarahisisha njia hii."
Matamshi haya yanakuja wakati ambapo uhusiano wa pande mbili kati ya Iran na China unaendelea kuimarika, hususan katika sekta za kiuchumi, miundombinu, nishati na ushirikiano wa kimataifa.
Kiongozi wa Mapinduzi ameweka wazi kuwa utekelezaji wa makubaliano hayo ya kina ndio msingi wa kuimarisha nafasi ya mataifa haya mawili katika mfumo mpya wa dunia unaojitokeza.
Your Comment