uwezo
-
Ripoti ya UNICEF, Sambamba na Siku ya Mtoto Duniani:
Gaza; Ardhi ya Mauaji Yasiyo ya Kawaida dhidi ya Watoto - Kila Dakika 17, Mtoto Huuwawa au Kupoteza Uwezo Fulani wa Mwili
Msemaji wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) amesema kuwa, “kila dakika 17 kwa wastani, mtoto mmoja au huuawa au kupoteza uwezo fulani wa mwili,” na kueleza takwimu hizi kuwa “hazikubaliki” na “zinazoshtua.”
-
Wizara ya Ulinzi ya Iran: Hakuna Nguvu Yenye Haki ya Kuingilia Uwezo wa Makombora ya Iran
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ulinzi, Brigedia Talaeinik alibainisha kuwa Marekani na washirika wake wanasisitiza mazungumzo kuhusu programu ya makombora na wanataka kupunguza umbali wa makombora ya Iran. Hata hivyo, alisema kuwa msingi wa uwezo wa makombora ya Iran ni kulinda usalama na maslahi ya kitaifa ya wananchi wake.
-
Bi Mujtahida Saffati: Vyuo vya kidini vya wanawake vinapaswa kuchukua uongozi wa kielimu wa wanawake katika ulimwengu wa Kiislamu
Profesa mashuhuri wa vyuo vya kidini vya wanawake, katika hafla ya uzinduzi wa mwaka mpya wa masomo, alivitaja “ikhlasi na uchamungu (taqwa)”, “kuungana na uongozi wa Kiislamu (wilaya)”, na “kuzingatia haki za wengine” kuwa ni nguzo tatu muhimu za mafanikio kwa wanafunzi wa fani za dini. Akaeleza kwa msisitizo kuwa: Taasisi za kielimu za wanawake zinapaswa kuchukua uongozi wa kielimu kwa wanawake wa ulimwengu wa Kiislamu, na kutumia uwezo huo kwa ajili ya kusambaza maarifa ya Kiislamu katika ulimwengu mzima wa Kiislamu.
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s): Uwezo wa Umma wa Kiislamu Unategemea Muunganiko wa Elimu na Imani
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) ameona kuwa muungano kati ya elimu na imani ni wa lazima, na akaeleza kwa kusisitiza kwamba: “Jamii ambayo inamiliki misingi hii miwili kwa pamoja – yaani elimu na imani - hufikia kiwango cha nguvu na mamlaka ambacho hakuna mfumo wowote wa kiutawala au ukoloni unaoweza kupenya ndani yake.”
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ataka Utekelezaji wa Makubaliano ya Kistratejia kati ya Iran na China
Ayatollah Khamenei amesisitiza nafasi ya kihistoria na ya kimkakati ya Iran na China katika bara la Asia na duniani, na akasema kuwa: "Iran na China, zikiwa na historia ya ustaarabu wa kale katika pande mbili za Asia, zina uwezo wa kuleta mabadiliko katika medani ya kimataifa na kikanda. Kuweka katika vitendo vipengele vyote vya makubaliano ya kistratejia, kutarahisisha njia hii."
-
Utekelezaji wa Majaribio wa Mpango wa "Shule Huru" katika Hawza ya Qom
Naibu Meneja wa Hawza ya Qom ametangaza kupitishwa kwa mpango wa “Shule Huru” na kuanza kutekelezwa kwa majaribio.
-
Zaidi ya Vikundi 200 vya Maombolezo vya Watu wa Mazandaran Wakiwa kwenye Haram ya Imam Ridha (a.s) / Mila ya Kihistoria ya Waombolezaji wa Kaskazini
Mkurugenzi wa Idara ya Tablighat Islami ya Mazandaran amesema: Mwaka huu zaidi ya vikundi 200 vya maombolezo kutoka miji mbalimbali ya mkoa huu, kwa hisia na ufahamu wa kipekee, vimeshiriki kwenye hafla za maombolezo na mikusanyiko ya kidini katika Haram ya Imam Ridha (a.s), na hivyo mila ya kihistoria ya watu wa Mazandaran imefanyika tena kwa upeo mkubwa.
-
Mashambulizi ya makombora ya Muqawama wa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu
Vyanzo vya habari vimeripoti shambulio la roketi kutoka Ukanda wa Gaza kwenye maeneo yanayokaliwa kimabavu ya Palestina.