Siku ya Kiyama
-
Darsa Fupi na Muhimu Katika Muktadha wa Maombolezo ya Bibi Fatimah az-Zahra (a.s) kuhusu "Fadhila na Siri za Tasbihat az-Zahra (a.s) na Ayatul Kursi"
Imam al-Baqir (a.s.) amesema: “Anayesema Tasbih ya Fatimah az-Zahra (a.s.) kisha akaomba maghfirah, atasamehewa. (Tasbih hiyo inaposomwa na mja) Ni mia moja kwa ulimi wake, lakini ni elfu moja katika mizani.”
-
Je, Raj‘a (kurejea kwa baadhi ya watu baada ya kifo kabla ya Kiyama):
Ni aina ya harakati ya kurudi nyuma na inayopingana na harakati ya kimaumbile (harakati ya kiasili ya kuendelea mbele) na mchakato wa ukamilifu?
Raj‘a, yaani kurejea kwa waumini waliokuwa wakamilifu kabisa na makafiri waliokuwa wabaya kabisa duniani katika kipindi cha kudhihiri kwa Imam Mahdi (a.s), ni ngazi miongoni mwa ngazi za Siku ya Kiyama, na imo katika njia ya ukamilifu wa mwanadamu.
-
Kumbukumbu Maalum:
Ukimya wa Kifo wa Nchi za Kiislamu; Asia ya Magharibi, “Palestina Mpya”
Kukubaliana kwa baadhi ya nchi za Kiislamu na mpango wa kinachoitwa mpango wa amani wa Trump kuhusu Palestina, ni alama ya aibu juu ya ulimwengu wa Kiislamu na baadhi ya viongozi wao wasio na imani ya kweli, na aibu hii haitafutika hadi Siku ya Kiyama.
-
Siku ya Wakati Maalum:
Ni ipi Maana ya Kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema kumwambia Shetani: "یوم الوقت المعلوم" “Siku ya Wakati Maalum"
katika ufahamu wa Shia (Wafuasi wa Ahlul-Bayt - a.s - ), "یوم الوقت المعلوم" ni Siku ya dhahiri ya Haki na Uadilifu wa Mwenyezi Mungu Duniani, yaani Siku ya Mapinduzi ya Dunia yakiongozwa na Imam Mahdi (a.t.f.s), kabla ya Siku ya Kiyama.