Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Likiinukuu Al Jazeera: Qatar imelaani shambulizi la "kiuoga" la Israel dhidi ya Hamas huko Doha.
Majed Al-Ansari, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, katika taarifa moja alisema kuwa nchi hiyo inalaani vikali shambulizi hilo ambalo, kwa mujibu wa maelezo yake, lililenga majengo ya makazi ya wanachama kadhaa wa ofisi ya kisiasa ya Hamas.
Katika taarifa hiyo imeelezwa:
"Shambulizi hili la kihalifu ni ukiukaji wa wazi wa sheria zote na kanuni za kimataifa, na ni tishio kubwa kwa usalama na afya ya wananchi wa Qatar na wakazi wake."
Serikali ya Qatar, sambamba na kulaani vikali shambulizi hilo, imesisitiza kuwa:
"Hatutavumilia tabia hii isiyo na akili ya Israel, uingiliaji wake wa mara kwa mara katika usalama wa kanda hii, na pia hatua yoyote itakayolenga kuhatarisha usalama na mamlaka ya Qatar."
Uchunguzi katika ngazi ya juu kabisa unaendelea, na maelezo zaidi yatatolewa mara tu yatakapopatikana.
Your Comment