27 Machi 2025 - 22:27
Siku ya Quds ni sehemu ya "Siku ya Kimataifa ya Uislamu"

Ayatollah Javadi Amoli, akiwaalika watu kushiriki katika Maandamano ya Siku ya Quds, alisema: Ni wajibu wetu sote kushiriki katika Maandamano haya, kwanza, Na kila mmoja wetu kwa mujibu wa elimu tuliyo nayo, awe na nia ya Tawalli na Tabarri ya Kimungu, pili, na kujaribu kufayanya kuwa maandamano mapana zaidi, tatu, yaani tuyafanye maandamano haya kwa nia ya kuwa karibu na kuwaheshimu na kuwathamini Mashahidi wa njia hii, ili hatua hizi zote zithibitishwe na Dhati Takatifu ya Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna -; Hazrat Ayatollah Javadi Amoli, katika ujumbe wake, alipokuwa akiwaalika watu kushiriki katika maandamano ya Siku ya Quds, alifafanua: Utaratibu wa matembezi ya Siku ya Quds, ambayo inachukuliwa kuwa moja ya Mila (Sunna) ya Ki-Mungu na ni moja ya kumbukumbu ya Imam Marhumu,  Ayatollah Imam Khomein (R.A), ni sio ibada ya kitaifa, ya kimadhehbu, ya kikanda, au rangi, au ya kikabila, bali hii ni sehemu ya "Tawalli na Tabarri ya Ulimwengu Mzima wa Kiislamu".

Nakala kamili ya ujumbe wa Mheshimiwa Ayatollah Javadi Amoli ni kama ifuatavyo:

Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

“Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote, na Sala na Salamu za Mwenyezi Mungu ziwashukie Manabii, Mitume, na Maimamu waongofu, na Fatima al-Zahra, tunawatawalisha na kuwafuata hao, na na maadui zao tunajitenga nao na kujikinga kutokana nao kwa Mwenyezi Mungu.

Maandamano ya Siku ya Quds, ambayo inachukuliwa kuwa moja ya Mila (Sunna) ya Ki-Mungu na ni moja ya kumbukumbu ya Imam Marhumu,  Ayatollah Imam Khomein (R.A), ni sio ibada ya kitaifa, ya kimadhehbu, ya kikanda, au rangi, au ya kikabila, bali hii ni sehemu ya "Tawalli na Tabarri ya Ulimwengu Mzima wa Kiislamu", Kwa sababu kwa upande mmoja, heshima na utakatifu wa Shule za Manabii wa Ibrahimu umevunjwa, na kwa upande mwingine, kauli na amri za viongozi wa Mwenyezi Mungu, Ibrahim Khalili-llah, Musa Kalimi-llah, na Yesu Kristo / Masih Issa (amani iwe juu yao wote) zimevunjwa.

Vitabu vyao vyote viwili vya mbinguni na kauli zao zenye kung'aa zimekiukwa, na utakatifu wa Qur'ani Tukufu haukuzingatiwa, na mchakato wa utumwa na kupaa juu ya uwepo uliobarikiwa wa Hadhrat Khatami Nabubat (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haukuzingatiwa.

Haki za aina hii ni haki za kimungu; Inahusiana na viongozi wa kiungu, inahusiana na mafunuo ya Mungu, na ni mwongozo wa Manabii. Kwa upande mwingine, ardhi ya watu wengine ilinyakuliwa kwa kujua na kwa makusudi, na watu wengi walinyang'anywa ardhi yao kwa zaidi ya miaka sabini, na dhulma ya wazi na mbaya imefanywa dhidi ya taifa kubwa, na jambo lingine ambalo linakumbukwa na limeongezwa katika ukatili huu na linazidi kuongezwa ni mauaji ya kimbari ya Israel, ambapo watoto, wanawake na watu wasio na hatia wameuawa kwa muda mrefu (kupitia utawala huo haram wa Israel). Tukio kama hili chungu, linakuwa tukio la ulimwengu wote na wajibu wa kila Mwanadamu ni kuwazingatia watu wanaodhulumiwa, kuungana nao, na kujitenga na watu madhalimu. 

Sasa kwa kuwa Sunna hii iliyoungwa mkono na iliyoasisiwa na Marhumu Imam Khomein (Mwenyezi Mungu Amrehemu) inafanyika, wazee wanaoshiriki katika maandamano haya, wanashiriki maandamano haya, ili kupata malipo ya kidunia na akhera; Maana yake ni kupata baraka za dunia na baraka za akhera; na hii inamaanisha kupokea baraka za kisiasa na kijamii pamoja na baraka za kidini na kiibada.

Majina haya yote yaliyotajwa yanapaswa kukusudia na kudhamiria kuwa karibu na kushiriki katika maandamano haya kwa kuheshimu shule za kimungu, kwa kuheshimu viongozi wa kimungu, kwa heshima ya Qur'an Tukufu, kwa kuheshima ya maneno ya Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao), kwa heshima ya Israa na Miiraji ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Mtiririko wa Tawalli na Tabarri, ni sehemu ya amri (na desturi)  rasmi za Kiislamu, (na Tawalli na Tabarri) zingine ni za maeneo maalum, zingine ni za ndani, zingine ni za kitaifa, na zingine ni za kimataifa.

Katika matembezi haya ya Quds, ili kunufaika na manufaa yote, tudhamirie kuwa karibu na anuani zote hizo, kwa sababu ikiwa ni kwa vitendo, na ikawa na mkusanyiko wa anuani kadhaa, basi kwa haki Mwanadamu ikiwa atakuwa na nia ya kuwa karibu na anuani zote hizo, atapata thawabu nyingi sana.

Wakubwa wanaoshiriki katika matembezi ya Siku ya Quds wasifikirie tu kwamba watoto, wanawake na watu wasio na hatia wa Gaza wanauawa, bali wanapaswa kulenga haya, kwamba wawe na lengo la kuikusudia Shule ya Manbii na Mitume wa zamani, kulenga na kuikusudia na kuiheshimu Njia ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, kulenga na kuheshimu utakatifu wa Qur'an Tukufu, kulenga na kuheshimu utakatifu wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), kulenga na kuheshimu utakatifu wa Israa na Miiraji, ili kwamba seti ya fadhila hizi iandamane na kuambatana na maanadamano haya matukufu.

﴿إِنَّ رَبَّکَ لَبِالْمِرْصَادِ﴾[۱]

Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu inanyemelea. Hakuna kinachopaswa kusemwa kwamba Israel, ambayo sasa inaungwa mkono na nchi za Magharibi na inaungwa mkono na Marekani, inaweza kuendeleza dhulma hii; Hii si kesi kamwe! Adhabu ya kimungu na ghadhabu Zake ziko karibu.


Kwa hiyo, ni wajibu wetu sote kushiriki katika maandamano haya, kwanza, na kila mmoja wetu kwa mujibu wa elimu tuliyo nayo, awe na nia ya Tawalli na Tabarri ya Kimungu, pili, na kujaribu kufayanya kuwa maandamano mapana zaidi, tatu, yaani tuyafanye maandamano haya kwa nia ya kuwa karibu na kuwaheshimu na kuwathamini Mashahidi wa njia hii, ili hatua hizi zote zithibitishwe na Dhati Takatifu ya Mwenyezi Mungu. Ili kuimarisha (na kuthabitisha) hatua hizi zote kwa Dhati Takatifu ya Mwenyezi Mungu; kokote uwapo duniani na katika Sarat, Inatarajiwa kwamba hatuautakayoipiga na kuichukua katika kushiriki maandamano haya kwa njia hii miguu yako haitateleza.

Watu wote, dada, kaka, na akina mama, watoto wote, wanaoshiriki katika maandamano haya (ya kimataifa ya Quds), wanapaswa kuzingatia anuani zote hizi na wasogee karibu (wajikurubishe karibu) zaidi na Mwenyezi Mungu, ili Dhati Tukufu ya Mwenyezi Mungu, inayoegemezwa na nia hizi safi na utakatifu maalum, iwajaalie thawabu za duniani na akhera, na hatimaye aweze kumtokomeza kwa upesi na haraka dhalimu muovu kama alivyosema:

﴿إِنَّ رَبَّکَ لَبِالْمِرْصَادِ﴾.

"Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu inanyemelea". 

Tunatumai kuwa mwaka huu wa 1404 Hijria - Shamsia (2025), mwisho wa dhulma dhidi ya watu wa Gaza na mwisho wa dhulma na udhalimu wa Israel utazingatiwa na utaratibiwa kwa baraka za uwezo na nguvu za Mwenyezi Mungu!

"Mwenyezi Mungu akupeni maghfira Yake, na amani iwe juu yenu, na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu"

[1]. Surah al-Fajr, Aya ya 14.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha