15 Julai 2025 - 23:55
Wananchi wa Yemen wanalenga (wanashambulia) maeneo mbalimbali ya Wazayuni kujibu jinai zinazoendelea kufanywa na Israel

Vikosi vya jeshi la Yemen vimeanzisha operesheni mpya ya ndege zisizo na rubani dhidi ya utawala wa Israel, hatua ambayo kwa mujibu wa duru za Yemen, ilifanyika kujibu mauaji ya raia huko Gaza.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Msemaji wa Jeshi la Yemen ametangaza utekelezwaji wa operesheni ya ndege zisizo na rubani dhidi ya maeneo yanayolengwa ya Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, na kutangaza kuwa shambulio hilo limefanywa katika kujibu kuendelea jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza.

Brigedia Yahya Saree, msemaji wa majeshi ya Yemen, alitangaza Jumanne usiku kupitia taarifa ya video kuwa vikosi vya Yemen vilitekeleza operesheni ya kijeshi ya pande mbili kwa wakati mmoja dhidi ya maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na utawala wa Kizayuni (Israel) kwa kutumia ndege tatu zisizo na rubani (droni).

Maelezo ya Operesheni kwa Muhtasari:

Droni mbili zililenga lengo muhimu la kijeshi katika eneo la Naqab.

Drone ya tatu ilishambulia bandari ya Eilat, kusini mwa ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Brigedia Saree alisisitiza kuwa operesheni hiyo ilifanyika kwa mafanikio na ilikuwa jibu kwa uhalifu unaoendelea kufanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Gaza, wakiwemo wanawake na watoto wanaouawa kila siku huku nyumba, mahema na miundombinu ya kibinadamu vikiharibiwa.

Kauli kuhusu Jumuiya ya Kimataifa: Alilaani kimya cha jumuiya ya kimataifa kuhusu mauaji haya ya kimbari, akisema kimya hicho kinawatia moyo wavamizi kuendeleza mipango yao ya kibeberu.

Ahadi ya Yemen: Akasema kuwa vikosi vya Yemen vinaendelea kutekeleza wajibu wao wa kidini, kimaadili na kihistoria, na operesheni za mashambulizi zitaendelea hadi uvamizi na mzingiro wa Gaza utakapoisha kabisa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha