Jarida la Marekani “The National Interest” katika makala yake ya uchambuzi limeonesha shaka kuhusu mafanikio ya mpango wa Donald Trump wa kuleta uthabiti wa kudumu katika Ukanda wa Gaza, na limeonya kuwa mpango huo unaweza kuchangia kuibuka kwa taasisi au kundi jipya linalofanana na Hezbollah katika eneo hilo.
Tabia ya ustahimilivu ya Iran na mhimili wa muqawama (mapambano ya upinzani) katika miongo iliyopita imeonyesha kuwa, licha ya mashinikizo na mashambulizi kutoka Marekani na utawala wa Kizayuni, Iran daima imeweza kujirekebisha kimkakati na kupata njia mpya za kukabiliana na changamoto.