Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sheikh Naeem Qasim, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, akizungumza kwa mnasaba wa kumbukumbu ya Allamah Sayyid Abbas Ali al-Mousawi (mjumbe wa Baraza la Kisheria la Baraza Kuu la Waislamu wa Kishia nchini Lebanon, mjumbe wa Bodi ya Wadhamini na miongoni mwa waasisi wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu Lebanon), alitathmini hali ya Lebanon na kusema: Mapambano ya “Fajr al-Joroud” yalikuwa mapambano yaliyoshirikisha jeshi la Lebanon na Muqawama wa Kiislamu, kwa uamuzi wa kishujaa wa Rais wa wakati huo Michel Aoun.
Akigusia kutoweka kwa Imam Musa al-Sadr, Sheikh Qasim alisema: “Imam Sadr alileta mageuzi ya kimsingi nchini Lebanon na alikuwa kiongozi wa wapiganaji. Alikuwa na mapenzi makubwa juu ya umoja wa kitaifa na aliamini kuwa Lebanon ya Kusini ilipigania niaba ya nchi nzima na Waarabu. Nasi pia tunafanya ahadi na Imam Sadr kwamba daima tutakuwa chini ya bendera ya Muqawama.”
Ameongeza kuwa mapambano ya Fajr al-Joroud yaliyoongozwa na jeshi la Lebanon kwa ushirikiano na Muqawama yameleta matunda makubwa. Uamuzi wa Michel Aoun kupambana na makundi ya kigaidi ya Daesh licha ya shinikizo la Marekani ulikuwa uamuzi thabiti na wa kishujaa. Aidha, katika mapambano hayo, Jenerali Joseph Aoun, aliyekuwa Kamanda wa Jeshi, alishirikiana kwa ukamilifu, na uratibu wa karibu kati ya jeshi na Muqawama ulifanikisha ushindi huo. Sheikh Qasim alisisitiza kuwa huo ni mfano bora wa mkakati wa ulinzi wa kitaifa.
Akizungumzia uvamizi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Yemen, alisema: “Israel imebombardhi Yemen na kama kawaida imewalenga raia na miundombinu ya kiraia. Israel inafanya uhalifu mbele ya macho ya dunia. Yemen imechukua msimamo wa kishujaa na wa kipekee katika kuunga mkono wananchi wa Gaza, na tunashukuru msimamo huo wa kiungwana.”
Kuhusu uamuzi wa serikali ya Lebanon kuondoa silaha za Muqawama, Katibu Mkuu wa Hizbullah alisema: “Kamwe hatutaweka chini silaha ambazo ndizo chanzo cha heshima, nguvu na ulinzi wetu dhidi ya adui. Kama si Muqawama, Israel ingeingia Beirut kama ilivyoingia Damascus, na ingetwaa kilomita 600 za ardhi ya Lebanon. Muqawama daima utabaki ngome madhubuti mbele ya ndoto za utawala wa Kizayuni.”
Aliongeza: “Uamuzi wa serikali wa kutaka kuondoa silaha za Lebanon umetokana na maagizo ya Marekani na Israel. Serikali ikiendelea na mkondo huu haitaweza kulinda mamlaka ya Lebanon. Silaha za Muqawama ni uhai, heshima, ardhi na izza yetu. Wanaotaka kuziondoa ni kama wale wanaotaka kuondoa roho zetu. Tukilazimishwa, dunia itaona msimamo wetu wa kijasiri.”
Sheikh Qasim alibainisha pia kuwa Muqawama ni mlinzi na msaidizi wa jeshi la kitaifa la Lebanon ambalo ndilo mhimili mkuu wa ulinzi wa nchi. Muqawama ni jibu la uvamizi wa adui na huzuia kufanikishwa malengo yake.
Aidha alisisitiza: “Israel inaweza kuvamia, kuua na kuharibu, lakini kamwe haitapata uthabiti. Kazi ya Muqawama leo ni kubwa zaidi na ya muhimu zaidi. Israel haiwezi kubaki Lebanon wala kutekeleza miradi yake ya upanuzi.”
Sheikh Qasim alieleza kuwa ramani ya njia ya baadaye ni: kufukuza adui kutoka ardhi ya Lebanon, kusimamisha uvamizi, kuwaachia huru wafungwa, kuanza upya ujenzi wa taifa na kisha kushughulika na mkakati wa ulinzi wa kitaifa.
Akikataa vikali sera ya kutoa ustaarabu mbele ya Israel, aliitaka serikali ya Lebanon ishikamane na makubaliano yake na Hizbullah, isitii shinikizo za nje, bali isimame kwa ujasiri na uwajibikaji.
Your Comment