26 Oktoba 2025 - 18:24
Majibu Makali ya Muqawama wa Iraq kwa Mjumbe wa Trump / Silaha za Muqawama Zimeleta Kujitolea Kukubwa Zaidi Ikiwemo Kufukuza Wavamizi

"Makundi ya Muqawama ni sehemu ya roho ya wananchi wa Iraq, na roho hiyo haiwezi kutenganishwa nao kwa uamuzi au matakwa ya wageni".

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- limeripoti kuwa vyombo vya habari vya Iraq vimeripoti majibu makali ya Muqawama wa Kiislamu wa Iraq kufuatia kauli za kuingilia mambo ya ndani zilizotolewa na mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump, kuhusu silaha za makundi ya Muqawama.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makundi ya Muqawama yamesisitiza kuwa uamuzi wao unategemea maslahi ya taifa la Iraq pekee.

Mjumbe huyo wa Trump katika masuala ya Iraq, Mark Sawia, aliyeteuliwa katika wadhifa huo siku sita zilizopita, alitangaza wazi kuwa “kipaumbele chake nchini Iraq ni kuvunja makundi ya Muqawama.” Kauli hiyo imefasiriwa kuwa ishara ya msimamo mkali zaidi wa serikali ya sasa ya Marekani ikilinganishwa na zile zilizotangulia.

Akiwa katika mahojiano, mjumbe huyo alisema kwa lafudhi ya kiukakamavu kwamba:

“Tutashirikiana na pande zote za Iraq kuhakikisha Iraq yenye nguvu inayoweza kuwa mshirika wa kweli wa Marekani – mbali na migogoro ya kikanda.”

Aidha, aliongeza kwa maneno ya kiburi:

“Nataka kuifanya Iraq kuwa kubwa tena, na ukurasa mpya wa ushirikiano sasa umeanza.”

Kauli hizo zilipokelewa haraka kwa majibu makali kutoka ndani ya Iraq.

Chanzo kimoja kilicho karibu na makundi ya Muqawama wa Iraq kiliiambia BAGHDAD AL-YOUM kwamba:

“Misingi ya kudumu ya Muqawama haitabadilika, awe ni mwakilishi wa Trump au mwingine.”

Chanzo hicho kilisisitiza kuwa maamuzi ya makundi hayo hutokana na maslahi ya taifa la Iraq na wala hayategemei matakwa ya mataifa ya Magharibi au Marekani.

Kimeongeza kuwa makundi hayo hayajali ripoti za vyombo vya habari vya Magharibi au Marekani, ambazo mara nyingi hujaa ujumbe uliopangwa au uliotiwa chumvi kwa lengo la kuchafua taswira yao mbele ya umma.

Kimebainisha pia kuwa makundi ya Muqawama yanashirikiana kwa karibu na serikali ya Iraq, na hakuna tofauti kubwa baina yao.

Chanzo hicho kilisisitiza kuwa:

“Silaha za makundi ya Muqawama ni mali ya Wairaqi, kwa ajili ya kulinda taifa dhidi ya uvamizi wa ndani au wa nje. Ni jambo lisilokubalika kwa taifa lolote la kigeni kuamua hatima ya silaha hizo.”

Kiliendelea kusema:

“Silaha hizo ndizo zilizochangia kujitolea kukubwa zaidi katika historia, zikiwemo kuwafukuza wavamizi, kupambana na magaidi na kukomboa miji iliyokuwa mikononi mwa magaidi.”

Mwisho, chanzo hicho kilihitimisha kwa kusisitiza kuwa: “Makundi ya Muqawama ni sehemu ya roho ya wananchi wa Iraq, na roho hiyo haiwezi kutenganishwa nao kwa uamuzi au matakwa ya wageni.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha