chanzo
-
Hashd al-Shaabi na Jeshi la Iraq washambulia maficho ya Daesh huko Rawah
Operesheni ya vikosi vya Hashd al-Shaabi kwa kushirikiana na Jeshi la Iraq dhidi ya mabaki ya kundi la Daesh katika eneo la Sahul, wilayani Rawah, magharibi mwa Anbar, imekumbwa na mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa na magaidi, ambapo mpiganaji mmoja wa Hashd al-Shaabi amejeruhiwa vibaya.
-
Kamanda wa Jeshi la Pakistan aelekea Tehran kwa mazungumzo na viongozi wa Iran
Chanzo cha kidiplomasia kimesema Kamanda wa Jeshi la Pakistan, Field Marshal Asim Munir, ameondoka Islamabad kuelekea Tehran kwa ajili ya kukutana na viongozi wakuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran: Mlango wa Hormuz Bado Haujafunguliwa, Hakuna Mabadiliko katika Sera ya Tehran
Chanzo cha kisiasa na kiusalama nchini Iran kimesema Mlango wa Hormuz bado haujafunguliwa, huku kikisisitiza kuwa Iran haijafanya mabadiliko yoyote katika sera na taratibu zake kuhusu upitishaji wa meli katika njia hiyo muhimu ya baharini.
-
Yemen: Jeshi la Yemen Ladai Limewasambaratisha Maafisa wa Saudi Arabia na Makundi Yake ya Kijeshi
Chanzo cha ngazi ya juu nchini Yemen kimesema kuwa mashambulizi ya vikosi vya Yemen dhidi ya maeneo ya Al-Mokha na Ma’rib yamelenga mikusanyiko ya maafisa wa Saudi Arabia pamoja na maghala ya silaha, huku kikisisitiza kuwa harakati zote za kijeshi za Saudi Arabia zinaendelea kufuatiliwa kwa karibu.
-
Kiongozi wa Yemen: Kulengwa kwa Meli ya Saudi Kumeimarisha Mlingano wa "Mzingiro kwa Mzingiro"
Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, Abdulaziz bin Habtour, amesema operesheni ya vikosi vya Yemen dhidi ya meli ya Saudi Arabia imethibitisha kuwa njia mbadala za kukwepa hatua zilizotangazwa na Yemen hazina usalama tena.
-
Chanzo cha kijeshi: Iran Ina Azma ya Chuma Kulinda Mamlaka Yake Katika Mlango wa Hormuz
Chanzo cha kijeshi kimenukuliwa na Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Kikisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina azma ya chuma katika kutekeleza mamlaka yake juu ya Mlango wa Hormuz na haitaruhusu eneo hilo la kimkakati kugeuzwa kuwa chanzo cha tishio dhidi yake.
-
Chanzo cha Kijeshi cha Iran:
Iran Itajibu Shambulio Lolote la Marekani Dhidi ya Miundombinu Yake kwa Kulenga Miundombinu ya Kimkakati Yenye Maslahi ya Marekani Katika Eneo
Chanzo cha kijeshi cha Iran kimesema kuwa iwapo Marekani italenga daraja au kituo chochote cha umeme nchini Iran, Iran itajibu kwa kulenga miundombinu na madaraja katika eneo hilo, ikiwemo vituo vya nishati ambavyo Marekani ina maslahi ndani yake. Chanzo hicho kimesema pia kuwa Marekani ilipaswa kutambua katika siku 10 zilizopita kwamba Iran ina uwezo wa kulenga eneo lolote itakaloamua kulishambulia.
-
Chanzo Chafichua Rasimu ya Vipengele 14 vya Makubaliano Yanayodaiwa Kupendekezwa kati ya Iran na Marekani
Chanzo kilicho karibu na timu ya mazungumzo ya Iran kimefichua rasimu ya makubaliano yenye vipengele 14 vinavyohusisha usitishaji wa uhasama, kuondolewa kwa vikwazo, kufunguliwa kwa Mlango wa Hormuz, pamoja na kuachiliwa kwa mabilioni ya dola za mali za Iran zilizogandishwa.
-
Iran Yajibu Shambulio la Marekani, Yalenga Kituo cha anga Kilichotumika Kushambulia Kisiwa cha Sirik
IRGC imesema imeharibu kituo cha anga kilichotumika katika shambulio dhidi ya mnara wa mawasiliano wa Kisiwa cha Sirik na kuonya kwamba mashambulizi yoyote yatakayojirudia yatakabiliwa na jibu kali zaidi.
-
Iran Yaongeza Ulinzi wa Mlango wa Hormuz, Vikosi vya Makombora Vapewa Mamlaka ya Kujibu Vitisho Moja kwa Moja
Chanzo chenye taarifa za ndani kimesema Iran imeimarisha kwa kiwango kikubwa uwepo wa kijeshi katika Mlango wa Hormuz, ikirejesha shughuli katika vituo vyote vya makombora vya eneo hilo na kupeleka vifaa vipya vya ulinzi vilivyofanikiwa kudungua makumi ya droni.
-
Ayatollah Mojtaba Khamenei Aonya Dhidi ya Njama za Kusababisha Mgawanyiko wa Kijamii Iran
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza umuhimu wa kulinda umoja wa wananchi, akionya kuwa adui anatumia mbinu za kueneza mifarakano ya kijamii baada ya kushindwa kufikia malengo yake kupitia mashinikizo ya kijeshi, kiuchumi na kisiasa.
-
Katika kikao cha kielimu “Mtume wa Rehema (s.a.w.w); Chanzo cha Msukumo wa Mazungumzo ya Kimataifa” ilisisitizwa:
Mtume Mtukufu (s.a.w.w) ni kielelezo cha maadili ya kibinadamu, mtangazaji wa umoja wa dunia na mbunifu wa ustaarabu wa Kiislamu
-
Wafanyakazi 741 wa sekta ya afya wameuawa au kujeruhiwa wakati wa vita vya Sudan
Mtandao wa Madaktari wa Sudan umetangaza kuwa tangu kuanza kwa vita nchini humo kati ya Jeshi la Sudan na Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) mnamo Aprili 2023, jumla ya wafanyakazi 234 wa afya wameuawa na 507 wengine wamejeruhiwa.
-
Shinikizo la Marekani kwa Baghdad; Makundi ya Muqawama: Hatufutiki kisiasa
Chanzo cha karibu na makundi ya Muqawama kilisema: “Muqawama na al-Hashd al-Shaabi pamoja na washirika wao wana angalau viti 97 bungeni, na wao ni sehemu isiyotenganishwa na mlinganyo wa kisiasa wa Iraq. Washington ilishindwa hapo awali kuyadhibiti makundi ya muqawama, na leo pia haitafanikiwa kwa vitisho vya kidiplomasia.” Chanzo hicho kiliongeza: “Sharti letu ni wazi; Waziri Mkuu awe huru, asiye tegemezi kwa Marekani, na anayewakilisha vipengele vyote vya nyumba ya taifa ya Iraq.”
-
Vita vya Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu si kwa sababu ya Nyuklia, bali ni kwa sababu ya Uenezi wa Ustaarabu Mpya wa Kiislamu
"Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni mkusanyiko wa damu zote zilizomwagika, subra, dhulma, mateso na juhudi za wanazuoni na Mashia katika historia nzima. Kuyaumiza mapinduzi haya ni sawa na kuumiza Uislamu kwa jeraha lisilopona kwa karne nyingi.”
-
Araghchi:
Balozi Mkuu wa Iran katika Van utafunguliwa / Chanzo kikubwa zaidi cha tishio kwa Syria ni kutoka kwa utawala wa Kizayuni
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema: Iran na Uturuki si tu nchi jirani, bali ni nchi mbili rafiki na ndugu zenye ushirikiano mkubwa sana.
-
Uzinduzi wa Mfumo wa Kielelezo cha Kujadiliana na Tafsiri za Qur’ani / Ayatollah Makarem:Teknolojia Mpya Iwe Kwenye Huduma ya Qur’ani na AhlulBayt(as)
Ayatollah Makarem Shirazi, mmoja wa maraja’ wa kiislamu, akisisitiza umuhimu wa kueneza habari za mafanikio ya kisayansi, alisema: “Moja ya mahitaji muhimu ya leo ni kuwafahamisha watu. Kuna shughuli nyingi zenye thamani zinafanyika, lakini taarifa zake ni chache. Vyombo vya habari, redio, televisheni na mashirika ya habari vinapaswa kusambaza maendeleo haya ili wananchi waone kiwango cha maendeleo ya teknolojia mpya katika sekta ya elimu ya dini.”
-
Majibu Makali ya Muqawama wa Iraq kwa Mjumbe wa Trump / Silaha za Muqawama Zimeleta Kujitolea Kukubwa Zaidi Ikiwemo Kufukuza Wavamizi
"Makundi ya Muqawama ni sehemu ya roho ya wananchi wa Iraq, na roho hiyo haiwezi kutenganishwa nao kwa uamuzi au matakwa ya wageni".
-
Kuendelea kwa Upanuzi wa Kijeshi wa Uturuki Ndani ya Ardhi ya Iraq
Vikosi vya uhandisi vya jeshi la Uturuki vimeanza kusimika minara ya mawasiliano ya kijeshi katika mlima wa Qandil uliopo mpakani mwa Iraq.