21 Juni 2025 - 22:04
Kuuawa Kishahidi kwa Abu Ali,Mkuu wa timu ya Ulinzi wa Shahidi Nasrullah, pamoja na «Sayyid Haidar Al-Muwa'li» Naibu wa Kataib Sayyid AlShuhadaa, Iraq

"Kwa Masikitiko, tumepata habari kuwa mmoja wa makamanda wa Kataib Sayyid al_Shuhada, Sayyid Haidar Al-Muwa'li, Naibu wa Abu A'la'i Al-Wila'yi, Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, amepata kifo cha Kishahidi wakati wa shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran."

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwakilishi wa Kataib Sayyid al_Shuhadaa nchini Iran amethibitisha kuwa Sayyid Haidar Al-Muwa'li, Naibu wa Abu A'la'i al_Wilayi, Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhadaa, ameuliwa na kufa kifo cha Kishahidi akiwa pamoja na Abu Ali, Msimamizi wa Ulinzi wa Sayyid Hassan Nasrallah, wakati wa shambulio la anga la utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.

Kuuawa Kishahidi kwa Abu Ali,Mkuu wa timu ya Ulinzi wa Shahidi Nasrullah, pamoja na «Sayyid Haidar Al-Muwa'li» Naibu wa Kataib Sayyid AlShuhadaa, Iraq

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) -ABNA- Sheikh Hassan Al-Iba'di, Mwakilishi wa Kataib Sayyid Shuhada nchini Iran, alieleza kwenye mazungumzo yake na Abna kuwa: "Kwa Masikitiko, tumepata habari kuwa mmoja wa makamanda wa Kataib Sayyid al_Shuhada, Sayyid Haidar Al-Muwa'li, Naibu wa Abu A'la'i Al-Wila'yi, Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, amepata kifo cha Kishahidi wakati wa shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran."

Akaendelea kusema: "Kulingana na taarifa za vyanzo vya kuaminika, walikuwa pamoja na Abu Ali Khalil, Msimamizi wa timu ya ulinzi wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, wote wawili walikufa Kishahidi wakati wa shambulio la kigaidi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha