Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran, Admiral Shahram Irani, amesema kuwa Muqawama sasa umevuka mipaka ya kijiografia, akisisitiza kuwa mataifa na vikosi vya Muqawama vinaendelea kuimarisha umoja na mshikamano katika kukabiliana na changamoto.
Kijana mmoja Msyria ameuliwa shahid usiku wa harusi yake wakati akipambana na uvamizi wa jeshi la Israel katika mji wa Bayt Jinn, ulioko katika vitongoji vya kusini mwa Damascus.
Katibu Mkuu wa Hezbollah Lebanon katika ujumbe rasmi kwa kiongozi wa Ansarullah Yemen, pamoja na kutoa rambirambi kwa kifo cha Rais wa Baraza Kuu la Jeshi la nchi hiyo, alithamini kujitolea kwake katika njia ya Quds na kupambana na maadui wa umma wa Kiislamu, na pia alimtakia mafanikio mrithi wake.