Kataib Hezbollah imeonya kuwa iwapo Marekani itaanzisha vita katika eneo hilo, itakabiliwa na hasara kubwa na vita vya muda mrefu, huku pia ikiutahadharisha utawala wa Kurdistan kuepuka kushirikiana na majeshi ya kigeni.
"Kwa Masikitiko, tumepata habari kuwa mmoja wa makamanda wa Kataib Sayyid al_Shuhada, Sayyid Haidar Al-Muwa'li, Naibu wa Abu A'la'i Al-Wila'yi, Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, amepata kifo cha Kishahidi wakati wa shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran."