27 Februari 2026 - 13:40
Onyo la Kataib Hezbollah Iraq kwa Marekani kuhusu Kuanzisha Vita katika Eneo

Kataib Hezbollah imeonya kuwa iwapo Marekani itaanzisha vita katika eneo hilo, itakabiliwa na hasara kubwa na vita vya muda mrefu, huku pia ikiutahadharisha utawala wa Kurdistan kuepuka kushirikiana na majeshi ya kigeni.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Harakati ya Kataib Hezbollah ya Iraq imetoa onyo kali kwa Marekani kuhusu madhara ya kuanzisha vita katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na Alsumaria, katika bayana yao wamesema kuwa wakati Marekani ikiendelea kutoa vitisho na kufanya harakati za kijeshi zinazoashiria kuongezeka kwa mvutano hatari katika eneo hilo, wanasisitiza umuhimu wa wanamapambano wao kuwa tayari kuingia katika vita vya muda mrefu vya kuchosha ambavyo vinaweza kuzidi makadirio ya serikali ya Marekani.

Kataib Hezbollah iliongeza kuwa iwapo Marekani itaanzisha vita katika eneo hilo, itakabiliwa na hasara kubwa ambazo zitakuwa vigumu kuzidhibiti au kuzifidia.

Katika taarifa hiyo pia, kundi hilo limeionya Serikali ya Mkoa wa Kurdistan ya Iraq kujiepusha na ushirikiano wowote na majeshi ya kigeni yenye uhasama, likisema kuwa hatua kama hiyo inaweza kuwa na madhara makubwa yanayoweza kutishia usalama na mustakabali wake.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha