Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Iraq ametangaza kufikiwa kwa makubaliano kati ya Tehran na Baghdad kuhusu kuyaondoa makundi yenye silaha yanayoipinga Iran katika eneo la Kurdistan, kaskazini mwa Iraq. Kwa mujibu wa tangazo hilo, makubaliano hayo yanahusu kuyafukuza makundi yanayotajwa kuwa yanavuruga usalama na mahusiano ya ujirani mwema, au kuyakabidhi kwa Iran.
Kataib Hezbollah imeonya kuwa iwapo Marekani itaanzisha vita katika eneo hilo, itakabiliwa na hasara kubwa na vita vya muda mrefu, huku pia ikiutahadharisha utawala wa Kurdistan kuepuka kushirikiana na majeshi ya kigeni.