Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (AS) -ABNA- Kituo cha habari “Asr” kwa mara ya kwanza baada ya shahada ya Sayed Hasan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hezbollah Lebanon, kimefanya mahojiano maalumu na binti yake wa pekee, Zainab Nasrallah. Mahojiano haya yameendeshwa na Hussein Pak, mwandishi wa habari na mtaalamu wa masuala ya Lebanon.
Zainab Nasrallah katika mazungumzo haya amezungumzia mambo ambayo hayakuwahi kusemwa kuhusu maisha binafsi ya baba yake kama mzazi, mume, na mtu wa kifamilia, na hivyo kutoa picha adimu kuhusu utu na haiba ya shahidi Syed Hasan Nasrallah.
Sehemu nyingine ya mahojiano haya imejikita katika mtazamo wake kuhusu mabadiliko ya karibuni nchini Lebanon na nafasi ya urithi wa baba yake katika fikra za wananchi wa eneo hili.
Wapenzi na wadau wanaweza kutazama mahojiano haya kamili kupitia tovuti rasmi ya kituo cha habari “Asr” kwa anuani: asrtv.com
Your Comment