31 Agosti 2025 - 00:27
Kukanushwa kwa Taarifa za Kuuawa kwa Abu Ubaidah / Onyo kutoka kwa Muqawama ya Kiislamu Kuhusu Uvumi

Muqawama ya Palestina yakanusha uvumi wa kuuawa kwa msemaji wa Brigedi za al-Qassam, Abu Ubaidah.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AhlulBayt (a.s) -ABNA- vikosi vya usalama vya Muqawama ya Palestina leo Jumamosi vilitoa taarifa ya kukanusha uvumi uliosambazwa na utawala wa Kizayuni kuhusu kuuawa kwa msemaji wa Brigedi za al-Qassam, Abu Ubaidah.

Muqawama ya Palestina imeonya dhidi ya kusambazwa kwa uvumi huu, ikisema chanzo chake ni utawala wa kigaidi wa Kizayuni, na kwamba uvumi huo unasambazwa kwa malengo maalum ya kijasusi.

Harakati ya Hamas imesisitiza kwamba vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vinaendeshwa chini ya maagizo ya jeshi na taasisi za kijasusi, na hakuna habari yoyote inayotolewa bila kibali cha kiusalama.

Muqawama imeongeza kuwa, kwa mujibu wa tajiriba iliyopo, utawala huo una tabia ya kusambaza uvumi kuhusu kuuawa kwa viongozi wa muqawama ili kuwafanya viongozi hao na mitandao yao ya mawasiliano kuchukua hatua fulani, hatua ambazo zitatoa taarifa muhimu zitakazotumiwa kwa ajili ya mashambulizi ya baadaye.

Hatimaye, Hamas imewataka wananchi kuwa waangalifu na kupuuza uvumi huo, ikieleza kuwa uvumi huo ni sehemu ya vita vya kisaikolojia vinavyolenga kudhoofisha umoja wa ndani wa wananchi wa Palestina.

Kukanushwa kwa Taarifa za Kuuawa kwa Abu Ubaidah / Onyo kutoka kwa Muqawama ya Kiislamu Kuhusu Uvumi

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha