6 Juni 2026 - 20:53
Marasimu ya Kumuenzi Ayatollah al-Udhma Al-Fayyadh Kufanyika Qum Usiku wa Leo

Ofisi ya Ayatullah al-Udhma Sistani mjini Qum imeandaa hafla ya kumuenzi marehemu Ayatullah al-Udhma Muhammad Ishaq al-Fayyadh, itakayofanyika baada ya Swala ya Magharibi na Isha usiku wa leo.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Hafla / Marasimu maalumu ya kumuenzi mwanazuoni mkubwa na faqihi mashuhuri marehemu Ayatollah Muhammad Ishaq al-Fayyadh itafanyika mjini Qom usiku wa leo.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hafla hiyo imeandaliwa na ofisi ya Marjaa Mkuu wa Kishia Grand Ayatollah Ali al-Sistani iliyoko Qum kwa lengo la kuenzi mchango mkubwa wa marehemu Ayatullah Al-Fayyadh katika nyanja za elimu ya Kiislamu, fiqhi na malezi ya wanafunzi wa dini.
 
Mkusanyiko huo utafanyika baada ya Swala ya Magharibi na Isha katika Uwanja wa Ruhullah mjini Qum, ambapo wanazuoni, wanafunzi wa hauza na waumini mbalimbali wanatarajiwa kushiriki kwa wingi katika kutoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wa marjaa wakubwa wa ulimwengu wa Kiislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha