Kundi la Wanazuoni wa Kiislamu, maimamu wa vituo vya Kiislamu na wajumbe wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa eneo la Metropolitan Washington walikusanyika Virginia kumuenzi Ayatollah al-Fayyadh na kuenzi mchango wake wa kielimu na kidini.
Ofisi ya Ayatullah al-Udhma Sistani mjini Qum imeandaa hafla ya kumuenzi marehemu Ayatullah al-Udhma Muhammad Ishaq al-Fayyadh, itakayofanyika baada ya Swala ya Magharibi na Isha usiku wa leo.