Marasimu
-
Hilali Nyekundu: Hakuna Majeruhi Walioripotiwa Katika Hafla ya Kuaga Kiongozi Shahidi Licha ya Mamilioni ya Waombolezaji Kushiriki
Shirika la Hilali Nyekundu limetangaza kuwa hadi sasa hakuna majeruhi walioripotiwa katika hafla ya kuaga Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, licha ya mamilioni ya waombolezaji kushiriki. Shirika hilo limeeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na usimamizi mzuri wa tukio hilo pamoja na ushirikiano wa wananchi.
-
Araghchi apongeza msimamo wa Jamhuri ya Congo wa kuiunga mkono Iran katika majukwaa ya kimataifa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi, ameishukuru Jamhuri ya Congo kwa msimamo wake wa kuendelea kuiunga mkono Iran katika majukwaa ya kimataifa, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo akiwasilisha salamu za rambirambi na mshikamano kwa taifa la Iran.
-
“Diplomasia ya Aya”: Aya za Qur'ani zilizosomwa katika marasimu ya mazishi ya Kiongozi Shahidi Imam Sayyid Ali Khamenei zavutia hisia za wengi
Katika marasimu ya kuuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei (Quds Sirruh), uteuzi wa Aya za Qur'ani Tukufu zilizosomwa kwa kila ujumbe wa wageni waliotoa salamu za rambirambi ulivutia hisia za wengi, huku kila Aya ikionekana kubeba ujumbe maalumu wa kisiasa, kiitikadi na kiroho.
-
Sheikh Shahriari: Kiongozi Shahidi aliliona umoja wa Umma wa Kiislamu kuwa nguzo ya kukabiliana na ubeberu wa maadui
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu, Hujjatul-Islam Hamid Shahriari, amesema kuwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei, alikuwa akiutazama umoja wa Umma wa Kiislamu kama mkakati wa msingi wa kukabiliana na ubeberu, uistikbari na njama za maadui za kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu.
-
Ratiba ya Hafla za Kuaga na Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Umma wa Kiislamu Yatangazwa
Ratiba rasmi ya hafla za kuaga, kuswaliwa na mazishi ya kiongozi shahidi wa Umma wa Kiislamu imetangazwa, huku shughuli hizo zikitarajiwa kufanyika katika miji ya Tehran, Qom na Mashhad.
-
Aref: Hafla za Kuaga na Mazishi ya Imam Shahidi Zitafanyika kwa Hadhi Inayolingana na Nafasi Yake ya Kihistoria na Kimataifa
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref, amesema maandalizi yanaendelea kuhakikisha hafla za kuaga na mazishi ya Imam Shahidi zinafanyika kwa ushiriki mkubwa wa wananchi na kwa hadhi inayostahili nafasi yake ya kihistoria na kimataifa.
-
Marasimu ya Kumuenzi Ayatollah al-Udhma Al-Fayyadh Kufanyika Qum Usiku wa Leo
Ofisi ya Ayatullah al-Udhma Sistani mjini Qum imeandaa hafla ya kumuenzi marehemu Ayatullah al-Udhma Muhammad Ishaq al-Fayyadh, itakayofanyika baada ya Swala ya Magharibi na Isha usiku wa leo.
-
Marasimu adhimu ya “Siku ya Shahidi” yafanyika Beirut
Sheikh Naeem Qassem: “Siku ya Shahidi si tu kwa ajili ya kuwakumbuka mashahidi, bali pia ni heshima kwa familia zao na wote wanaounga mkono njia ya mapambano ya muqawama.”