Chanzo cha kijeshi kimenukuliwa na Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Kikisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina azma ya chuma katika kutekeleza mamlaka yake juu ya Mlango wa Hormuz na haitaruhusu eneo hilo la kimkakati kugeuzwa kuwa chanzo cha tishio dhidi yake.
Wizara ya Ulinzi ya Israel imetiliana saini mkataba mkubwa na Kampuni ya Rafael ili kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa makombora ya kukinga ya mfumo wa Iron Dome (Gombo la Chuma).
Mheshimiwa Ayatollah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, usiku huu katika hotuba ya televisheni akiwahutubia watu, aliueleza umoja na mshikamano wa kudumu wa taifa la Iran kuwa ni ngumi ya chuma juu ya kichwa cha adui.