umoja wa kitaifa
-
Jukumu la Marajii wa Kidini wa Kishia katika;
"Kulinda Umoja wa Kitaifa na Utambulisho wa Iran / Sehemu ya Saba: Kisa cha Kuokolewa kwa Lugha ya Taifa ya Iran na Ukombozi wa Azarbaijan"
Kulinda umoja wa ardhi na kuzingatia utambulisho wa kidini ni miongoni mwa masuala yaliyokuwa yakipewa umuhimu mkubwa na viongozi wa kidini katika ardhi za Kiislamu. Kiasi kwamba kila aina ya uvamizi au shambulio dhidi ya ardhi za Kiislamu ilikabiliwa na mwitikio mkali kutoka kwao. Uvamiuzi wa Azarbaijan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na juhudi za kuutenga mkoa huo kutoka Iran ni miongoni mwa mambo yaliyodhihirisha tena ushawishi wa uongozi wa kidini katika kulinda umoja wa ardhi ya nchi. Aidha, kulinda utambulisho wa kitaifa wa Kiairani pia lilikuwa ni mojawapo ya masuala yaliyopatiwa umuhimu maalum na viongozi (Marajii) wa kidini katika kipindi cha utawala wa Pahlavi.
-
Kiongozi wa Mapinduzi katika hotuba ya televisheni kwa taifa la Iran:
''Umoja wa Kitaifa wa Iran ni ule ule wa Tarehe 13 Juni 2009; Wote wanawajibika''
Mheshimiwa Ayatollah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, usiku huu katika hotuba ya televisheni akiwahutubia watu, aliueleza umoja na mshikamano wa kudumu wa taifa la Iran kuwa ni ngumi ya chuma juu ya kichwa cha adui.
-
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa jukumu la UNIFIL nchini Lebanon hadi mwisho wa mwaka 2026.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuongeza muda wa jukumu la wanajeshi wa UNIFIL kusini mwa Lebanon kwa mara ya mwisho.
-
Rais wa Iran: Mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran Yameleta Umoja wa Kitaifa Usio na Mfano
"Leo tunashuhudia kwa macho yetu kuwa kila Muirani - awe ni mfuasi wa Serikali au mpinzani wake - amekuwa sauti moja katika kutetea hadhi, uhuru, na mamlaka ya nchi yetu".
-
Sayyid Ali Khamenei: "Utawala wa Kizayuni haukufikiria kamwe kupokea mashambulizi kama haya kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu".
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu - Leo akihutubia Taifa la Iran, ametoa ufafanuzi mzuri mno wa matukio yalivyojiri, na kauli imara za kutia moyo kwa wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambazo kwa hakika zimeonyesha mshikamano wa kitaifa, ujasiri, na kukataa kuachia madikteta au nguvu za kigeni na kibeberu kutawala na kuidhibiti Kijeshi Mashariki ya Kati. Pia, kauli za Kiongozi huyu imara na mwenye busara na hekima ya hali ya juu, zinaonyesha msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya nje, na kutotetereka katika suala zima la kuifyekelea mbali mikono ya adui yeyote yenye nia ovu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.