Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Licha ya madai ya Rais wa Marekani kuhusu kufanikisha makubaliano yatakayopelekea amani na kumalizika kwa vita katika eneo hili (la Mashariki ya Kati), dunia bado inashuhudia mlolongo wa vita vinavyoendelea, hasa katika eneo la Asia ya Magharibi (Mashariki ya Kati). Kuanzia vita na machafuko nchini Syria na uvamizi wa ardhi ya nchi hiyo, hadi kuongezeka kwa mzingiro wa Gaza na idadi kubwa ya mashahidi katika eneo hilo.
Kwa upande mwingine, mazungumzo ya Marekani na Urusi pamoja na mashauriano ya nchi za Magharibi na Iran hayakuzaa matunda ya amani. Hali hiyo ni matokeo ya tamaa kubwa ya NATO, nchi za Magharibi, Marekani na Israel, ambayo inaongezeka siku hadi siku.
Mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Yemen pia yameonesha kuwa hakuna chaguo jingine isipokuwa upinzani wa moja kwa moja dhidi ya mhimili wa uovu wa Kimagharibi-Kiamerika na Kizayuni, ili kuzuia uvamizi wao dhidi ya mataifa mbalimbali na kujenga uwezo wa kuzuia (deterrence) wa kweli.
Katika muktadha huu, Abbas al-Zaydi, mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Iraq na mwanachama wa Harakati ya Hashd al-Shaabi, ameandika makala yenye kichwa:
"Operesheni za Ujanja kwa Mtindo wa Kimarekani – Vita Vinavyoitwa Amani"
Yeye anaeleza:
Marekani, kwa jina la "amani", imekuwa ikiendesha vita vyake dhidi ya dunia kwa njia mbalimbali – muhimu zaidi ikiwa ni kutumia:
-
NATO
-
Israel
-
Magenge ya kigaidi.
Mazungumzo hayo na hatua hizo huwasilishwa kama juhudi za kidiplomasia au “ubunifu wa kisiasa”, lakini kila mtu mwenye akili timamu anaelewa kwamba Washington inaongoza vita hivi dhidi ya:
-
Urusi
-
Iran
-
Ukanda mzima wa Mashariki ya Kati
Aidha, mauaji ya halaiki huko Gaza, mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Lebanon na Yemen, na juhudi za kudhoofisha mfumo wa kisiasa nchini Iraq ni sehemu ya mkakati huu.
1. Urusi:
Marekani na washirika wake wanaendeleza vita dhidi ya Urusi kwa njia zifuatazo:
-
NATO na Umoja wa Ulaya wanaandaa mazingira ya vita dhidi ya Urusi.
-
Kuvuruga ushirikiano wa kijeshi/kisiasa kati ya Urusi na Iran au hata Urusi na China.
-
Kufungua front mpya dhidi ya Urusi, kama vile nchini Georgia.
-
Kupanua NATO kwa kuongeza wanachama wapya – hasa mataifa jirani na Urusi.
-
Kuweka ushuru au vikwazo kwa wanaoagiza mafuta na gesi ya Urusi (mfano India).
-
Kupindua serikali zinazoshirikiana na Urusi, mfano Venezuela.
-
Kutafuta njia mbadala za biashara ya kimataifa, kama ushirikiano wa kiuchumi kati ya Armenia na Azerbaijan, na kushinikiza Pakistan.
-
Kudhamini na kuendesha magenge ya kigaidi dhidi ya nchi zinazolengwa.
2. Iran:
Mazungumzo ya nyuklia na Iran yamefungua mlango wa kila aina ya uwezekano – kutoka vita vifupi vya siku 12 hadi athari pana kwa Iran, mhimili wa muqawama, eneo na dunia.
Marekani imeendeleza mbinu za kuizingira Iran licha ya mazungumzo:
-
Trojka ya Ulaya imeanzisha tena "mekanizimu wa trigger" ili kupeleka hali kwenye mgogoro mkubwa.
-
Kufungua front mpya dhidi ya Iran, hasa kupitia Azerbaijan (ambayo ni tishio kubwa).
-
Kukatilia mbali matawi ya Iran katika Lebanon, Yemen, na Iraq – baada ya kuudhibiti Syria.
-
Kuchochea uhasama kati ya Iran na majirani zake.
-
Kudhamini vikundi vya kigaidi na vuguvugu la kutaka kujitenga ndani ya Iran.
-
Kuongeza vikwazo vya kiuchumi.
Muhtasari:
-
Urusi haitasalimika kutokana na vita na mashinikizo yanayoongozwa na Marekani. Tunatarajia kufunguliwa kwa front mpya nje ya uwanja wa Ukraine katika kipindi cha kati.
-
Iran ni shabaha kuu ya Marekani na Israel, na hawatarudi nyuma. Pande zote mbili – Iran kwa upande mmoja na Marekani/Israel kwa upande mwingine – wanaona vita hii ni ya kimaamuzi na ya hatima.
-
Eneo la Mashariki ya Kati linabakia kuwa kwenye mgogoro mkali, liko karibu kulipuka, na bado halijatulia.
-
Muungano kati ya Iran, Urusi na China ni dhaifu, hauna ujasiri wa kutosha, na haujafikia kiwango cha mshikamano kama wa Marekani na Ulaya. Kwa hivyo, hauwezi kuhimili hatari na changamoto kubwa zinazolikabili.
Your Comment